Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w74 3/15 kur. 143-144
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1974
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1974
w74 3/15 kur. 143-144

Maswali Kutoka kwa Wasomaji

● Wakati wa ubatizo, ni mavazi gani yanayofaa kwa mwanamke?​—U.S.A.

Biblia haisemi kwamba ama mwanamume ama mwanamke amepaswa avae vazi la pekee wakati wa ubatizo. Kwa hiyo ni juu ya mwanamke kuamua analofikiria kuwa linafaa. Wanawake wengi wanaona kwamba vazi la kuogelea la kadiri linatumika vema kwa kusudi hilo. Katika sehemu nyingine za ulimwengu wanawake wanavaa kanga au vazi refu (kama joho). Bila shaka, katika kuchagua atakachovaa wakati wa ubatizo wake, imempasa mwanamke aukumbuke uzito wa wakati huo. Kwa wazi isingefaa kwake kuvaa vazi la kuogelea ambalo lingefikiriwa kuwa la kupita kadiri na lenye kufunua uchi sana. Wala asingevaa kanga yenye kushikamana na mwili isivyofaa inaposhika maji. Kupatana na 1 Timotheo 2:9, uchaguzi wake umepaswa uonyeshe “adabu nzuri, na moyo wa kiasi.”

● Samweli wa Pili 11:4, 5, NW, anasema: “Daudi akapeleka wajumbe ili amtwae [Bath-sheba]. Kwa hiyo akaingia kwake naye akalala naye, alipokuwa akijitakasa na uchafu wake. . . . Naye mwanamke huyu akachukua mimba.” Je! “uchafu” huu unamaanisha mwezi na, ikiwa ndivyo, Bath-sheba angewezaje kuchukua mimba wakati huo?​—U.S.A.

Biblia haisemi kabisa uchafu huo ulikuwa nini ambao Bath-sheba alijitakasa nao. Pengine ulishirikiana na kipindi chake cha mwezi au na kutoka kwa namna ya majimaji au na jambo jinginelo lote lililoleta uchafu wa kawaida. Watafsiri wengine hata wanayatafsiri maneno haya katika njia ya kushauri kwamba alijitakasa na uchafu uliotokana na ngono yake na Daudi. Tafsiri ya Kijeremani iliyofanywa na Leander van Ess yasema: “Naye akamjia, naye akalala naye. Naye akajitakasa na uchafu wake, naye akarudi nyumbani kwake.” Kulingana na tafsiri hii Bath-sheba aliitimiza sheria ya Mambo ya Walawi 15:18: “Huyo mwanamke naye ambaye mtu mume amelala naye kwa shahawa, wote wawili wataoga majini, nao watakuwa najisi hata jioni.”

Hata hivyo, kwa kuwa utakaso wa uchafu ulikamatana na kawaida ya mwezi ya Bath-sheba, angaliweza bado kuchukua mimba. Kulingana na Mambo ya Walawi 15:19, 29, mwanamke aliyekuwamo katika kipindi cha mwezi alikuwa mchafu kwa siku saba (zikihesabiwa tangu mwanzo wa kutoka kwa majimaji yake) naye alipaswa kujitakasa siku ya nane. Kama mwanamke angeweza kuchukua mimba siku ya nane ingetegemea kawaida yake, ambayo si yenye muda mrefu sawasawa katika wanawake wote. Ikiwa Bath-sheba alikuwa na kawaida ya katikati ya siku 21 na 26 urefu wake, angaliweza kuchukua mimba siku ya nane ya kawaida yake. Kwa mfano, kwa habari ya kawaida ya siku 21 mimba yaweza kuchukuliwa kwa sababu ya ngono iliyofanywa siku ya tatu (tukihesabu tangu mwanzo wa kutoka kwa damu) mpaka siku ya kumi.

● Mnamo vita ya pili ya ulimwengu, katika kambi fulani za mateso katika Ujeremani ambapo wanawake peke yao walifungiwa, kulikuwako visa ambapo dada aliye wakf alibatiza. Hivyo, dada mmoja asimulia kwamba nyuma ya alipokuja kwenye ujuzi wa kweli katika kambi ya mateso na kujiweka wakf kwa Yehova ndipo yeye alipobatizwa na dada. Je! ubatizo huu unafaa?​—Ujeremani.

Uchunguzi wa Biblia hauonyeshi ushuhuda wo wote wa wanawake wakibatiza. Lakini una maandishi ya mifano ya wanaume walio wakf wakibatiza wengine. (Mt. 3:13-17; Yohana 4:2; Matendo 8:38) Sisi hatuamriwi na Neno la Mungu kutangaza kwamba ubatizo uliofanywa na dada unakubalika; kwa hiyo, katika kisa kilichotajwa, yampasa dada huyo abatizwe na ndugu aliye wakf kulingana na matakwa ya Biblia.

Lakini, hii haimaanishi kwamba wakf uliofanywa na dada huyo katika kambi ya mateso haufai. Uhakika wenyewe wa kwamba angali akimtumikia Yehova nyuma ya kufunguliwa kwake kutoka kambini waonyesha kwamba alijua alikuwa anafanya nini naye alikuwa amefanya wakf kweli kweli. Kwa hiyo, tarehe ya wakf wake yaweza kuandikwa naye kama hapo kwanza.

Mtu akijifunza kweli anapokuwamo gerezani au mahali penginepo pote pasipo na wanaume walio wakf wa kubatiza naye mtu huyo ataka kufanya wakf kwa Yehova, nini kiwezacho kufanywa? Warumi 10:10 yasema: “Kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.” Mwanamke anayeamini aweza kumfikia Yehova kwa sala na kufanya wakf. Ndipo anapoweza kuikiri imani yake waziwazi naye aweza kuwaeleza akina dada walio wakf wawezao kuwapo kwamba ‘ametumia imani moyoni mwake’ na kwamba anangoja nafasi ya kwanza abatizwe na ndugu. Yehova anautazama moyo (Mit. 17:3; 21:2), na kwa kweli hali ya moyo ya mwanamke kama huyo ingeongoza kwenye wokovu. Kwa habari ya Kornelio na nyumba yake, kwa wazi kulikuwako ufahamu wa kimbinguni wa hali ya moyo, kwa maana roho takatifu iliwaangukia mbele ya ubatizo. Ndugu sita waliotahiriwa kutoka Yafa walikuwa wamefuatana na Petro wakati huo nao wasingeweza kupinga hata kidogo Petro alipoamuru waamini hawa wa kwanza wa Mataifa waliokuwa wamepokea roho takatifu wabatizwe.​—Matendo 10:44-48.

Vivyo hivyo, huenda mwanamume akajifunza kweli na kufanya wakf ulio halali anapokuwa amefungwa gerezani, na ijapokuwa wapo akina ndugu walio wakf, angali anazuiwa asibatizwe kwa maana maji ambayo ni ya lazima hayapatikani. (Yohana 3:23; Matendo 8:36) Yeye vile vile aweza kuifuata kawaida iliyoonyeshwa juu.

Kwa hiyo kuna njia iliyo wazi kwa wanaume na wanawake vile vile wasio na njia ya ubatizo, ama kwa sababu hali haziuruhusu ama kwa sababu mwanamume aliye wakf hayupo. Lakini kwa kufanya wakf ulio halali na kuja waziwazi mbele ya wengine walio wakf waliopo mwanamume huyo au mwanamke anakubaliwa sasa kama aliye wakf. Lakini haielekei kufaa kwa kulingana na Maandiko kwa dada kujaribu kubatiza.

Kwa habari ya ubatizo, huenda vile vile ikasemwa kwamba ubatizo waweza kufanywa na mwanamume aliye wakf ingawa wasiwepo mashahidi wo wote wa kibinadamu. Zipo kanuni za Maandiko katika visa vya Yesu na towashi Mwethiopia za kuonyesha hivi. Na kwa kuwa sala inatolewa ifaavyo mbele ya uzamisho, sikuzote wapo mashahidi wa kimbinguni.

Yapaswa ikumbukwe sikuzote kwamba lililo la muhimu zaidi kupita yote ni kutimiliza wakf wa mtu nyuma ya unapomaliza kufanywa.

● 1 Wakorintho 7:1 inamaanisha nini inaposema, “Ni heri mwanamume asimguse mwanamke”?​—U.S.A.

Maneno haya ya mtume Paulo yanatanguliza mazungumzo yanayopendekeza kukaa bila ya kuoa ama kuolewa kama zawadi bora kuliko ndoa kwa wale walio na kujiweza na wanaojitahidi kujitoa wenyewe kabisa kusudi waiendeleze ibada ya kweli. (1 Kor. 7:6-9) Linapotumiwa katika njia inayofanana na hiyo katika Maandiko ya Kiebrania, neno “kugusa” linamaanisha ngono. Kwa mfano, kwa habari ya mkewe Ibrahimu, Sara, Yehova alimwambia hivi Abimeleki: “Nikakuzuia usinitendee dhambi, kwa hiyo sikukuacha umguse. Basi sasa umrudishe mwanamke kwa mtu huyo.” (Mwa. 20:6, 7) Vile vile, Mithali 6:29 inaonyesha ngono kuwa kitu kimoja na “kugusa”: “Ndivyo alivyo aingiaye kwa mke wa jirani yake; kila mtu amgusaye huyo atakuwa na hatia.”

Kwa kupatana na matumizi ya Biblia ya neno “kugusa,” maneno ya Paulo juu ya ‘kutomgusa mwanamke’ yanafungamana na kuepuka kuonea tamaa au ngono. Ndoa ndiyo njia ya pekee yenye heshima ambayo mtu anaweza kuwa na mgusano huo. Kwa kuwa ndivyo ilivyo, Paulo, alipoandika kwamba “ni heri mwanamume asimguse mwanamke,” alikuwa akisema kwamba ni jambo lenye kufaidi kwa Mkristo kukaa bila ya kuoa, nayo An American Translation na New Testament ya Weymouth inayatafsiri maneno hayo kwa njia hiyo. Mtume aliendelea kueleza jambo hili.

Ni jambo linalostahili kuangaliwa kwamba onyo la ‘kutomgusa mwanamke’ vile vile linalifuata onyo kali la kuepuka uasherati. (1 Kor. 6:15-20) Wakati mmoja Yesu Kristo alisema hivi: “Mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.” (Mt. 5:28) Hivyo yaweza kuonekana kwamba hata kwa mwanamume kumtazama mwanamke kwa kumwonea tamaa ni kosa. Kama angeipata nafasi, angetimiliza kwa matendo tamaa ya uzinifu ya moyo wake. (Linganisha 2 Samweli 11:2-4.) Kwa kuongeza, basi, ‘kumgusa mwanamke’ kunaweza kutia na mgusano wo wote wa kimwili unaoletwa na nyege au unaochochea nyege, kwa maana hii inakuwa zaidi ya kutazama.

Kwa hiyo, mwanamume anayetaka kukaa bila ya kuoa kwa njia ya heshima amepaswa aepuke matendo yote yawezayo kuchochea nyege au kuongoza kwenye uasherati. Akiona ni vigumu mno kufanya hivyo, ni afadhali zaidi aoe. Aliandika mtume Paulo: “Kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe.”​—1 Kor. 7:2.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki