Safina ya Nuhu Si Chombo Kidogo
● Safina ambayo Mungu alimwamuru Nuhu aunde huenda mara nyingine ikadhaniwa kuwa chombo kidogo. (Mwa. 6:14, 15) Lakini makala ya karibuni juu ya vyombo vikubwa vinavyochukua mafuta inasema sivyo: “Ile safina ilipaswa iwe mojawapo ya vyombo ambavyo ni vikubwa zaidi kuliko vyote ili ipate kuelea juu ya bahari, urefu wake ilikuwa futi 450, futi 75 upana wake na futi 45 urefu wa kwenda juu. Hii ilikuwa kubwa zaidi kuliko vyombo vingi vya miti vyenye kujulikana sana vilivyoundwa tangu wakati wa Nuhu na ilipita hata meli nyingi za kwanza za vyuma zenye kuendeshwa na nguvu ya mvuke, hivyo kumstahilisha Nuhu kama fundi mkubwa kuliko wote wa waundaji wa meli—ingawa pia yapaswa idhaniwe kwamba yeye alipokea msaada zaidi kutoka kwa chanzo cha juu zaidi.”—Oil Lifestream of Progress, Namba Tatu, 1973.