Fadhili Ni Yenye Nguvu
● Fadhili yaweza kuvunja hata upinzani mkali sana. Haya ndiyo yaliyokuwa maono ya mtu aliyepooza katika Philippines. Mkewe alipinga vikali asijifunze Biblia na mashahidi wa Yehova. Watoto hata wakatisha kwamba akiwa Shahidi wao wasingemwona tena kama baba yao. Jamaa, ambao alikuwa akiishi katika uwanja wao, wakamwambia aondoke katika ardhi yao. Mashahidi wa Yehova katika eneo lake wakaja haraka kumsaidia. Wakamsaidia kuhamia mahali pengine na wakati ule ule wakafanya matengenezo upya. Wonyesho huu wa fadhili ulikuwa na matokeo gani juu ya mkewe na watoto wake? Walivutwa waanze kujifunza Biblia. Sasa wote ni Mashahidi waliobatizwa.