Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w76 7/15 kur. 317-320
  • “Ishara ya Milele”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Ishara ya Milele”
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1976
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1976
w76 7/15 kur. 317-320

“Ishara ya Milele”

Makala hii ni ya kutumia kwa mafunzo ya kitabu ya kundi

1. Usemi unaotumiwa katika fungu la Isaya 55:13 ambalo maneno yake yametumiwa hapa waonyeshaje kurudishwa kwa baraka ya Mungu juu ya watu wake?

SASA, utazamie ushuhuda unaoonyesha kurudishwa kwa baraka ya Mungu juu ya watu wake wenye kuabudu waliokuwa wamemtafuta na waliokuwa wameitia jina lake kwa kutubu na kwa tunda la haki linalofaa toba! “Badala ya michongoma utamea msunobari, na badala ya mibigili, mhadesi.” (Isa. 55:13) Badala ya mimea midogo yenye kuchoma inayotakiwa kuepukwa, yamea miti ambayo majani yake huwa mabichi sikuzote, kama mhadesi na msunobari unaokua kufika urefu wa futi 65 (kama metre.20). Huko ndiko ndege wa angani, hata korongo, wawezako kufanya makao yao. (Zab. 104:16, 17) Waisraeli waliorudishwa wangeweza kutwaa matawi yenye majani kutokana na mhadesi wajijengee vibanda wakati wa kuadhimisha sikukuu ya vibanda (au, hema) wakati wa juma ya tatu ya mwezi wa Tishri. (Neh. 8:15, 16; Zek. 1:8-11) Lo! ni kiburudisho, kipendeza macho gani kutokana na miti ambayo majani yake huwa mabichi sikuzote kama msunobari na mhadesi, badala ya mimea yenye kuchoma, yenye kuwasha!

2. Eleza maana ya ahadi hii: “miti yote ya kondeni itapiga makofi” na “mbele yenu milima na vilima vitatoa nyimbo.”

2 Ilikuwako miti mingine ya kuipamba nchi iliyolimwa tena. Kwani, “miti yote ya kondeni itapiga makofi.” Itamsifu Muumba wao wa kimbinguni, anayeikuza. Pamoja na majani mengine yenye maua-mwitu, itaifunika mitelemko ya milima na vilima. Sura ya miinuko hii ya nchi ya Yuda itachangamka. Itasimulia ujumbe wa kumsifu Mungu, na itakuwa kana kwamba inatoa sauti za “nyimbo.” Mazingira ya asili yanakuwa yenye furaha, yakionyesha Mungu akikufurahia kurudishwa kwa watu kwenye uhuru wa kuabudu katika Yerusalemu na katika nchi yote ya Yuda. (Isa. 55:12) Wakazi wa nchi hii iliyogeuzwa wangewezaje kuacha kujichangamsha na kutoa kelele za kumshukuru na kumsifu Yeye?

3, 4. (a) Sura ya nchi iliyokaliwa tena ingemwongoza mtu ailinganishe na nini? (b) Mungu alikuwa amemwongoza Ezekieli atabiri nini juu ya jambo hilo?

3 Ule uzuri uliotazamiwa kuipamba nchi iliyokaliwa tena ungeweza kumfanya mtu aulinganishe na ule wa Bustani ya Edeni, makao ya kiparadiso ya kwanza ya wanadamu. Sasa watazamaji wa mpambo wa nchi ambayo wakati fulani ilikuwa ukiwa wangefanya ulinganifu huo. Jambo kama hilo lilitabiriwa katika unabii ambao Mungu alimwongoza Ezekieli atoe baada ya kuharibiwa kwa Yerusalemu na hekalu lake katika mwaka wa 607 K.W.K. na nchi ya Yuda ikaanza kuwa ukiwa.

4 “Bwana [Yehova] asema hivi; Siku ile nitakapowatakaseni na maovu yenu yote nitaifanya miji ikaliwe na watu, na palipobomolewa pajengwe tena. Nchi iliyokuwa ukiwa italimwa, ijapokuwa ilikuwa ukiwa mbele ya macho ya watu wote waliopita. Nao watasema, Nchi hii, iliyokuwa ukiwa, imekuwa kama bustani ya Adeni; nayo miji iliyokuwa mahame, na ukiwa, na magofu, sasa ina maboma, inakaliwa na watu. Ndipo mataifa, waliobaki karibu yenu pande zote, watajua ya kuwa mimi, [Yehova], nimejenga mahali palipoharibika, nami nimepanda mbegu katika nchi iliyokuwa ukiwa; mimi, [Yehova], nimesema hayo; tena [nimeyatenda].”​—⁠Eze. 36:33-36.

5. Jina la Mungu mwenyewe, sifa yake, ilitiwaje katika mambo yaliyokuwa yakitukia kwa watu wa Israeli?

5 Hakuna mtu ambaye angaliweza kubadili mambo haya kwa ajili ya taifa la Israeli lililochukiwa na mataifa yote na kuhamishwa isipokuwa Mungu wao, aliyekuwa akishika agano lake pamoja nao. Hivyo, kwa kufanya hivi kulingana na ahadi yake, alikuwa amejifanyia mwenyewe sifa katika dunia yote. Jina lake, sifa yake, fahari yake, ilitiwa katika jambo hili lenye maana sana, kwa maana watu waliohusika na kugeuka kwa matukio haya walikuwa watu walioitwa kwa jina lake mwenyewe. Lililowapata lilileta sifa nzuri au sifa mbaya juu ya jina lake. Mashauri yenye makosa ambayo watu wa Mataifa walikuwa wamekata kwa namna alivyoadhibu watu wake wa agano yalipaswa yasahihishwe. Hii ingehusu namna mataifa yasiyo ya Kiyahudi walivyomwona kama mungu mdogo tu. Kwa kujiheshimu mwenyewe na kwa staha yake mwenyewe ilikuwa lazima athibitishe kwa mataifa yote kwamba yeye alikuwa Mungu wa kweli, mwenye kutegemeka, mwenye kushika ahadi!

6. (a) Kusudi lake la kwanza katika kurudisha watu wake Israeli kwenye nchi yao lilikuwa nini? (b) Lilikuwa jambo gani lililowezesha kugeuza nchi hiyo Iwe paradiso?

6 Aliwakomboa katika Babeli wa kale akawarudisha kwenye nchi alikokuwa ametoa kipindi cha sabato cha miaka 70, si kwanza kwa ajili ya watu wake Israeli wa agano, bali kwa ajili ya jina lake mwenyewe. (Law. 26:41-45; 2 Nya. 36:20, 21) Kipindi hiki cha sabato kilipokwisha, katika mwaka wa 537 K.W.K., ndipo alipowarudisha walimaji wa halali wa nchi hiyo. Kwa kuwabariki, aliigeuza kuwa nchi yenye kupendeza, ambayo sura yake ikawa karibu na ile ya Paradiso ya Furaha, Bustani ya Edeni. Hili lilikuwa na maana kuu. Lilikuwa na kusudi.

7. Kusudi la hili lilikuwa nini, kama inavyosemwa katika Isaya 55:13?

7 Mungu anajulisha kusudi la hili, mwenyewe akisema hivi: “Jambo hili litakuwa la kumpatia [Yehova] jina, litakuwa ishara ya milele isiyokatiliwa mbali.” (Isa. 55:13) Kupambwa huku kwa nchi iliyokuwa ukiwa kwa muda mrefu na uzuri wa kiparadiso kulifanya watu wa Mataifa waliokuwa wakitazama wakubali kwa wivu na kukafanya wamheshimu sana.

8. Katika kufahamu “ishara” inayotajwa katika Isaya 55:13, jambo gani lapaswa likumbukwe juu ya nchi na wakazi wake?

8 Wakati nchi ilipokuwa huko, ikiwa imelimwa na kutukuzwa, ilikuwa “ishara” ya jambo fulani lenye maana sana. Kwanza, na ikumbukwe kwamba ilikuwa nchi iliyopewa na Mungu, kwa maana Yehova alikuwa amewapa watu wake wateule nchi hiyo katika karne ya kumi na tano K.W.K.,kwa utimizo wa ahadi yake aliyofanya kwa babu zao Ibrahimu, Isaka na Yakobo (au Israeli). Ndipo, kwa sababu ya kuendelea kutokutii na kutoaminika kwa watu wake, ilikuwa kana kwamba ameipindua nchi kama nyungu na kuwatoa wakazi wayo, akiwahamisha kuwapeleka kwenye nchi ya Babeli na kuruhusu nchi iliyochafuliwa kuwa ukiwa katika kushika sabato kwa muda wa miaka 70. (Isa. 24:1-6; 2 Fal. 21:13) Na sasa alikuwa amezalisha tena nchi yenye kukaliwa na watu na pia akazalisha tena taifa kwa kurudisha watu wake waliokuwa wamehamishwa kwenye nchi yao waliyopewa na Mungu. Basi, kugeuzwa kwa nchi iwe paradiso kungekuwa “ishara” kwa heshima ya nani?

9. (a) Kugeuzwa kwa nchi kuwa paradiso kulikuwaje “ishara” iliyomheshimu Yehova? (b) Ni nini limeifanya iwe “ishara ya milele”?

9 Yehova mwenyewe atoa jibu la kweli kupitia kwa kinywa cha nabii wake Isaya, akisema: “Na hili litamfanya Yahweh kuwa mwenye sifa, ishara milele, isiyofutika.” (Isa. 55:13, The Jerusalem Bible) Au, “Yote haya yatampatia BWANA jina kuu, lisiloharibika, ishara kwa wakati wote.” (The New English Bible) Kwa habari Yake inakanusha kwamba “Mungu amefariki.” Kazi zake za ajabu juu ya nchi hiyo zilithibitisha kwamba Yeye ni Mungu aliye hai, ni kwamba unabii uliotolewa kwa jina lake Yehova ni wa kweli. Jina alilojifanyia hivyo lilikuwa kuu na lenye utukufu. Na ile nchi ya Yuda iliyo kama paradiso, iliyokaliwa watu tena ilikuwa “ishara” ya Uungu wake, ya enzi yake kuu ya ulimwengu wote, ya uweza wake, ya uaminifu wake, na ya rehema yake iliyojuu kama mbingu kwa watu wenye kutubu waliokuwa katika agano pamoja naye. Hii ikawa “ishara ya milele,” hata sasa; ni ishara ambayo ‘haikukatiliwa mbali,’ hata majeshi ya Kirumi yalipokwisha kuharibu Yerusalemu wakaiharibu nchi ya Yuda katika mwaka wa 70 wa Wakati wetu wa Kawaida. Kwa sababu gapi sivyo? Kwa sababu maandishi ya kutimiza kwa Mungu unabii wake yameandikwa katika maandishi yasiyoharibika ya Biblia.

10. (a) Mfano wa kisasa wa “ishara” hiyo tunaupata ukiwa na watu gani? (b) Hali ya nchi yao ya mfano ilikuwaje wakati wa kukombolewa kwao katika Babeli Mkuu?

10 Kwa sababu hii ni ishara isiyoharibika, isiyofutika, “ya milele,” twatafuta mfano wake wa kisasa. Ili kupatana na mfano wa kale, hii ingetia mabaki ya kisasa ya Israeli wa kiroho walio katika “agano jipya” kupitia kwa Mpatanishi Mkubwa Zaidi, Yesu Kristo. Historia ya kisasa yathibitisha kwamba mabaki haya yalikombolewa katika Babeli Mkuu, ile milki ya ulimwengu ya dini ya uongo, katika mwaka wa 1919 W.K. Hali yao ya kidini au ya kiroho duniani ilikuwa imeharibiwa sana na uharibifu waliofanyiwa wao, pia tengenezo lao la kazi na Babeli Mkuu na wasaidizi wake wa kisiasa, wa kijeshi na wa kisheria. Nchi yao ya mfano, ya kiroho, ilikuwa kana kwamba imepigwa marufuku kwa sababu mambo yaliyokuwa kama michongoma na mibigili yaliharibu sura yake. Haikutoa sura yenye kuvutia ambayo ingekaribisha watu wenye kupenda dini washiriki na waabudu hawa wa Yehova Mungu imani na matendo yao.

11. Yehova alipowafungulia njia ya kurudi kwao, mabaki ya Israeli wa kiroho yaliitikiaje?

11 Walakini, Mungu wao aliye hai alipowafungulia njia, ilikuwa “kwa furaha” kwamba mabaki ya Israeli wa kiroho ‘wakatoka’ katika utumwa wa Babeli Mkuu. Walijaa tumaini, wakiziona nafasi za kidini za wakati ujao ijapo walifahamu ingetaka uhodari kuzitumia katikati ya ulimwengu wenye uadui. Vita ya dunia yote ilikuwa imemalizika na kukawa kumekuwa na amani ya muda, na hivyo ilikuwa “kwa amani” kwamba ‘wakaongozwa’ kuletwa katika nchi yao ya kiroho ya halali, kurudishwa kwao kwenye kibali ya Mungu, kupatanishwa kwao naye, kukubaliwa kwao tena wamtumikie kama mabalozi wa ufalme wake wa Kimasihi ambao sasa ulikuwa umesimamishwa. (2 Kor. 5:20) Wakajitayarisha wafanye kazi iliyokuwa mbele iliyokuwa imetabiriwa na Yesu Kristo ifanywe wakati wa “mwisho wa taratibu ya mambo,” yaani: “Habari njema hizi za ufalme zitahubiriwa katika dunia yote inayokaliwa na watu kwa ushuhuda kwa mataifa yote; na ndipo ule mwisho utakapokuja.” Wakaanza kuyaondoa mambo yaliyokuwa yenye kukataliwa na yenye kuzuia ibada ya kweli ya Mungu.​—⁠ Mt. 24:14, NW.

12. Paradiso ya kiroho ulimwenguni pote imefanyizwaje ikaliwe na watu wa Mungu katika nyakati za kisasa?

12 Akiwa mwaminifu kwa ahadi zake zilizoandikwa na kwa kupatana na mfano wa kale, Yehova alizibariki jitihada za mabaki waliorudishwa wa Israeli wa kiroho. Paradiso ya kiroho imetokea, ambayo ni ajabu ulimwenguni pote leo. Ni kama milima na vilima vya nchi yao ya kiroho vilikuwa vimewachangamkia mbele yao kwa nyimbo, na kana kwamba miti ya uzaaji wa Kikristo ilikuwa ikipiga makofi yao. Kwa njia ya mfano, msunobari wenye kupendeza na mhadesi wenye majani mabichi sikuzote ikawa badala ya michongoma na mibigili. Sura yake ya kulaaniwa na Mungu imetoweka! Imekuwa mahali penye kukalika kwa Wakristo wa kweli, wanaofuata sana mfano wa Mtumishi aliyetiwa mafuta wa Yehova, Yesu Kristo. Wako pia mamia ya maelfu ya watu wenye kupenda haki waliokuwa wakimtafuta Yehova, Mungu wa mabaki yaliyorudishwa ya Israeli wa kiroho. Hawa wamekuwa wenzi wenye kushikamana wa mabaki yenye uaminifu waliotiwa mafuta.

13. Nchi iliyopambwa ya mabaki ya kiroho imekuwaje “ishara” inayomheshimu Yehova, na “isiyokatiliwa mbali”?

13 Mgeuzo huu wa ajabu wa nchi ya kiroho ya mabaki umetokeza sifa kwa Yehova katika dunia yote. Jina la Mungu mwenyewe limejulikana kuzunguka dunia yote. Nchi iliyorudishwa na kupambwa, ya mabaki ya kiroho, imekuwa “ishara,” na itaendelea milele. Imeendelea mpaka sasa ijapokuwa Vita ya Ulimwengu ya Pili na matata na misiba mingine ya ulimwengu. ‘Haijakatiliwa mbali’ mpaka sasa, na haitakatiliwa mbali kamwe.​—⁠Isa. 55:12, 13.

14, 15. Katika shauri hili la kurudishwa kwa Israeli wa kiroho, ilitokeaje kama inavyosemwa katika Isaya 55:8, 9?

14 Hasa hili limekuwa la ajabu, lenye kustaajabisha sana machoni pa mabaki yaliyorudishwa ya Israeli wa kiroho. Wakati wa maonezi ya Vita ya Ulimwengu ya Kwanza na wakati wa utumwa wao kwa Babeli Mkuu, hawakupata kuwaza kamwe kwamba jambo hilo lingetukia. Kulingana na walivyoufahamu unabii wa Biblia wakati huo, jambo hilo lilikuwa lisilowezekana! Ingalifikiriwa kuwa kuwazia tu kutazamia au kutabiri jambo hilo kutukia kwa mabaki haya waliokuwa watumwa, wahamishwa wa Israeli wa kiroho ambao wangali duniani. Bila shaka mawazo yao hayakulingana na mawazo ya Mungu wala njia zao hazikulingana na njia zake. Ikawa sawasawa na ambavyo Yehova mwenyewe alivyosema:

15 “Mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema [Yehova], Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.”​—⁠Isa. 55:8.

16. Ushuhuda wote waonyesha nani amefanyiza paradiso hii ya kiroho?

16 Yote yaelekea kuonyesha kwamba jambo hili si la mwanadamu, bali ni la Mungu Mwenye Nguvu Zote. Leo kanuni iliyosemwa na mwanasheria Gamalieli kwa Baraza Kuu ya Yerusalemu katika siku za mitume wa karne ya kwanza W.K., ni ya kweli katika habari hii: “Shauri hili au kazi hii ikiwa imetoka kwa binadamu, itavunjwa, lakini ikiwa imetoka kwa Mungu hamwezi kuivunja.” (Matendo 5:38, 39) Kwa hiyo, ile paradiso ya kiroho ambayo haikukatiliwa mbali itoke kwa mashahidi wa Yehova wa Kikristo mpaka leo hii ni “ishara” ambayo Mungu Mwenye Nguvu Zote amefanyiza. Kupitia kwayo amekuwa mwenye sifa sana duniani pote. Amejipatia mwenyewe jina kuu. Watu wote wale wenye kumwogopa Mungu ambao wametimiza matakwa ya kuingilia paradiso ya kiroho ambayo yeye amesimamisha kwa kumtafuta wakati angali aweza kupatikana na kuitia jina lake mwenyewe wakati angali yu karibu wakati wa huu “mwisho wa taratibu ya mambo,” wanaweza kuwa wenye kushukuru.​—⁠Isa. 55:6; Mt. 24:3, NW.​—⁠Kutoka Kitabu Man’s Salvation Out of World Distress at Hand!, sura ya 7.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki