“Wakati wa Jua Kupunga”
◇ “Wakati wa jua kupunga” [kwa halisi, wakati wa roho au upepo] ndipo Yehova alipotangazia Adamu na Hawa waasi hukumu yao katika Edeni. (Mwa. 3:8-19) Pengine alifanya hivyo kabla ya jua kutua, wakati ambao pepo baridi zenye kuburudisha zinapotokea katika jimbo ambako Bustani ya Edeni yadhaniwa ilikuwa. Mahali hapo pako mashariki ya Uturuki, karibu maili 140 (kilomita 225) magharibi ya kusini ya Mlima Ararati na maili chache kusini ya Ziwa Van.