Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w77 6/1 kur. 259-260
  • Furaha ya Mataifa Yote Afrika Kusini

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Furaha ya Mataifa Yote Afrika Kusini
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1977
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1977
w77 6/1 kur. 259-260

Furaha ya Mataifa Yote Afrika Kusini

MWAKA 1973 Mashahidi wa Yehova walikuwa na kusanyiko la mataifa yote katika Afrika Kusini. Kwanza, karibu watu 1,000 kutoka Afrika Kusini walikwenda nchi za mbali wakahudhurie makusanyiko ya mataifa yote katika Ulaya, Uingereza na United States of America. Shauku yao ilisaidia kusanyiko lao wenyewe la mataifa yote katika Johannesburg lifanyiwe bidii nyingi. Kwa mara ya kwanza Afrika Kusini ikawa kati ya nchi zenye kuwa na makusanyiko ya mataifa yote nao walitazamia wageni kutoka Ulaya na sehemu nyingine za ulimwengu.

Akina ndugu walipanga kuwe na makusanyiko matatu mbalimbali, moja la ndugu weupe, moja la ndugu machotara na Wahindi, na moja la ndugu Waafrika. Walikuwa wakipanga kuunganisha makusanyiko yote matatu Jumapili alasiri wakati wa kipindi kimoja, kwa maana walijua wasingepewa ruhusa ya kuwa na kusanyiko la mwungano siku zote. Lakini walipata magumu.

Kwanza, hawakupewa ruhusa ya kuwa na kusanyiko la Waafrika Johannesburg. Kwa hiyo makusanyiko ya Waafrika yalipangwa mahali patano mbalimbali. Hivyo watu wa Yehova hawakushindwa, bali hiyo ilikuwa baraka kwao, kwa maana ndugu wengi Waafrika ambao wasingaliweza kuhudhuria waliweza kuwa na pesa za kuhudhuria kusanyiko la karibu zaidi.

Lakini yalikuwako magumu zaidi. Idara ya Mambo ya Ndani haikupendelea Mashahidi wa Yehova kwa sababu ya suala la kijeshi lililokuwamo nchini. Kwa hiyo, wengi waliotazamiwa kutembelea sehemu hiyo wakihudhuria kusanyiko la Mashahidi wa Yehova walikatazwa vyeti vya kuingia nchini. Kati yao alikuwa mwangalizi wa tawi la Amerika, Milton Henschel, na katibu mweka-hazina wa Sosaiti, Grant Suiter. Ndugu wa Afrika Kusini walikata sana tamaa.

Walakini, bado makusanyiko yalipata ushindi wa kimungu! Ndugu wengi kutoka Ulaya walifika kama watalii wakafurahia ushirika mzuri na ndugu wa Afrika Kusini. Kusanyiko la Waafrika lililopaswa kuwa Johannesburg lilipelekwa Benoni, mji ulio karibu maili 20 kuelekea mashariki ya Johannesburg. Jumapili, Januari 6, 1974, programu ilianza saa 3 ya asubuhi na kumalizika saa sita adhuhuri. Mipango yote ilifanywa mapema, na kati ya saa sita adhuhuri na saa tisa alasiri ndugu wote waliokuwa katika makusanyiko mawili ya Johannesburg na lile la Benoni walikuja Rand Stadium katika Johannesburg kuhudhuria vipindi vya mwisho vilivyounganishwa. Kila mtu alistaajabu jinsi walivyohama katika sehemu zile tatu wakaja Rand Stadium, bila mvurugo. Walifika Rand Stadium kwa motokaa, bas na gari-moshi, nao waliendelea tu kumiminika hata uwanja ukajawa na watu​—jumla ya wenye kuhudhuria ikawa 33,408. Wengi walisimama.

Hiyo ilikuwa hali yenye kupendeza Mashahidi wa Yehova kweli kweli, kuona ndugu zao Waafrika, Machotara na weupe wakishirikiana pamoja kumwabudu Yehova. Hakukuwa na ubaguzi wa rangi. Waliojua Kiingereza wangeweza kuketi po pote, nao akina ndugu walitumia nafasi hiyo kuketi na ndugu zao wa mataifa mengine. Waliopendelea Kizulu wangeweza kuketi sehemu ya Kizulu; wenye kusema Kisesotho, katika sehemu ya Kisesotho. Zilikuwako pia sehemu za Kiafrikaans na Kireno. Lilikuwa kundi lenye mchanganyiko na kila mtu alifurahi sana. Kwa kweli, walifurahi sana hata ikawa vigumu kuwazuia waache kupiga makofi kupita kiasi. Ndugu hawajapata kuwa wenye furaha hivyo, na wengi wanasema hiyo ilikuwa alasiri “isiyosahaulika.”

Iliwezekanaje? Walikuwa wamekodi uwanja huo mmoja katika Johannesburg kwa ajili ya makusanyiko ya mataifa yote, nao hawakujua walifanya hivyo kwa uongozi wa kimungu! Ruhusa haikuhitajiwa ili kuwe na kipindi hicho kimoja. Jumla ya waliohudhuria hotuba ya watu wote katika makusanyiko yote ya “Ushindi wa Kimungu” ‘ilikuwa watu 56,286, na 1,867 walibatizwa.​—1976 Yearbook.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki