Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w79 6/1 uku. 24
  • Yehova Afunua Hukumu Zake

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yehova Afunua Hukumu Zake
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
w79 6/1 uku. 24

Yehova Afunua Hukumu Zake

Yehova Mungu hawafishi watumishi wake hukumu zake. Kitabu cha Biblia cha Amosi kinatuambia hivi: “Hakika Bwana [Yehova] hatafanya neno lo lote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake. Simba amekwisha kunguruma, ni nani asiyeogopa? Bwana [Yehova] amenena, ni nani awezaye neno ila kutabiri?​—Amosi 3:7, 8.

Uchunguzi wa maandishi ya Biblia unaonyesha wazi kwamba watumishi wa Mungu ndio waliokuwa wa kwanza kujua lile alilokusudia kufanya. Noa ndiye aliyekuwa wa kwanza kujua kwamba ulimwengu usiomwogopa Mungu ungeharibiwa katika gharika ya dunia yote. Ibrahimu aliambiwa maoni ya Yehova juu ya Sodoma na miji iliyouzunguka, nao manabii Waisraeli walijulishwa mara kwa mara mambo ambayo yangetukia katika wakati ujao. Hilo liliwawezesha manabii hao kutoa onyo, na kuwasihi Waisraeli waache njia zao za uasi.

Mngurumo wa simba ni milio wa onyo, unaoogopesha wale wanaousikia. Vivyo hivyo, Yehova aliposema, na kufunua hukumu zake kwa manabii wake, hilo liliwafanya watende. Hilo liliwasukuma watabiri, watangaze yale waliyokuwa wamejulishwa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki