Mwujiza Unaolingana na ‘Ufufuo.
Akiwa na umri wa miaka 99, Ibrahimu alikuwa mzee sana asiweze kuzaa mtoto. Lakini umri wake mkubwa haukuwa kizuizi kikubwa cha kumzuia Muumba asiweze kumrudishia uwezo wake wa kuzaa, na kumwezesha kumzaa Isaka kupitia kwa mkewe mpendwa Sara ambaye vilevile alirudishiwa nguvu zake za uzazi. (Mwa. 17:17; 21:1, 2; Rum..4:19) Kwa kuwa mwujiza huu ulihusiaha na kurudishwa kwa chembe zenye uhai, kweli. kweli ulilingana na Ufufuo. Kwa kushangaza, kurudishwa huku kwa uwezo wa Ibrahimu wa kuzaa watoto hakukuwa kwa kitambo tu. Baada ya kifo cha Sara, Ibrahimu alipochukua mke mwingine Ketura, alizaa wana wengine sita—Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki Sua. Hivyo zaidi ya miaka 40 baada ya Ibrahimu kurudishiwa nguvu zake bado alikuwa na uwezo wa kuzaa. (Mwa. 23:1; 25:1, 2) Hilo laonyesha vizuri sana yale aliyoambiwa bikira Mariamu na malaika Gabrieli karne nyingi baadaye: “Hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu.” (Luka 1:37) Vilevile mwujiza huo unatoa uthibitisho kuhusu uhakika wa tumaini la ufufuo.