Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w79 9/15 uku. 19
  • Neno la Mungu Launganisha Jamaa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Neno la Mungu Launganisha Jamaa
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
w79 9/15 uku. 19

Neno la Mungu Launganisha Jamaa

Ripoti kutoka Jamhuri ya Dominica inaeleza juu ya afisa wa kijeshi ambaye jamaa yake ilikaribia sana kuvunjika. Alitumwa Ufaransa, lakini, kwa sababu ya magumu ya fedha, akalazimika kuituma jamaa yake United States. Walakini, upesi, mwanamume huyo alianza kuwa na uhusiano wa karibu sana na wanawake wengine. Yeye anaeleza hivi:

“Baada ya muda nilifahamu kwamba nilikuwa nikifanya jambo baya nayo dhamiri yangu ilianza kunisumbua. Kwa hiyo mimi nami nilikwenda United States. Huko, nilimwomba Mungu anisaidie.

“Nilisikia juu ya mikutano iliyokuwa ikifanyiwa karibu na nyumbani. Kwa hiyo nilimpeleka mke wangu pamoja na wale watoto wachanga zaidi mahali hapo. Palikuwa Jumba la Ufalme la Mashahidi wa Yehova. Upesi funzo lilianzishwa pamoja nasi nami nikafanya maendeleo haraka sana. Nilipoanza kujifunza kutoka katika Biblia juu ya maisha ya jamaa, nilitumia mambo hayo. Upesi jamaa yetu iliyogawanyika ikaungana. Tukawa wahubiri wa Ufalme, na sasa tumerudi nyumbani hapa katika Jamhuri ya Dominica, tukiwa wenye furaha na kuridhika.”

Wakati mmoja, mwanamume huyu alikuwa mwenye kupiga ubwana naye hakuwa mnyenyekevu hata kidogo. Walakini, sasa, yeye ni Mkristo anayetumikia kwa unyenyekevu katika mojawapo la makundi ya Mashahidi mjini Santo Domingo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki