Kutimizwa kwa Neno la Mungu ni Hakika
Yehova Mungu alimwambia Ibrahimu hivi: “Kwa habari za Ishmaeli nimekusikia, nimembariki, nitamzidisha, nami nitamwongeza sana sana. Atazaa [wakuu] kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa kuu.” (Mwa. 17:20) Wakati huo Ishmaeli mwana wa Ibrahimu alikuwa mwenye umri wa miaka 13. (Mwa. 16:16; 17:1) Hakuna mwanadamu ye yote ambaye angeweza kutabiri kwamba kijana huyo aliyekuwa bado kuoa angekuwa baba ya wakuu 12. Walakini Muumba mwenye hekima yote alitabiri. Vyanzo viwili vya kihistoria vimehifadhi utimizo wa ufunuo huo wa kimungu, vikitaja wakuu 12 wafuatao: Nebayothi, Kedari, Abdeeli, Mibsamu, Mishma, Buma, Masa, Hadadi, Tema, Yeturi, Nafishi na Kedema. (Mwa. 25:13-15; 1 Nya. 1:29-31) Jambo hilo linaonyesha kwa nguvu uhakika wa kutimizwa kwa neno la kiunabii la Mungu!