Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w82 8/15 uku. 8
  • Je! Kwa Kweli Jina Hilo Ni La Maana?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Kwa Kweli Jina Hilo Ni La Maana?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
  • Habari Zinazolingana
  • Kwa Nini Ni Lazima Tujue Jina la Mungu
    Jina la Mungu Litakaloendelea Milele
  • Mungu Anaitwa Nani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu Wote)—2019
  • Jinsi ya Kujua Jina la Mungu
    Amkeni!—2004
  • Jina la Mungu na Lako
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
w82 8/15 uku. 8

Je! Kwa Kweli Jina Hilo Ni La Maana?

HILO ndilo ulizo ambalo wengi wanauliza kunapokuwa mazungumzo juu ya jina la Mungu. “Mungu ni Mungu,” ndivyo wanavyosema. “Kwa hiyo kwa sababu gani tuhitaji jina?”

Kitabu The Illustrated Bible Dictionary, kilichochapishwa katika 1980 na Tyndale House Publishers, kinatoa maelezo haya juu ya umaana wa jina katika nyakati za Biblia: “Uchunguzi juu ya neno ‘jina’ katika AK [Agano la Kale] unaonyesha jinsi [Jina] linavyomaanisha mengi katika Kiebrania. Jina si kibandiko tu, lakini ni lenye maana ya utu halisi wa mwenye [Jina] hilo. Laweza kutokana na hali za kuzaliwa kwake (Mw. 5:29), au kuonyesha tabia yake (Mw. 27:36), na wakati mtu anapoliweka ‘jina’ lake juu ya kitu au mtu mwingine yeye anakuja chini ya uongozi na ulinzi [wa mwenye jina] hilo.”

Halafu, kuhusu jina la Mungu, Dictionary (Kamusi) hiyo inasema: “Kwa hiyo, Yahweh, tofauti na Elohim [Mungu], hasa ni jina la mtu, ingawa Mtu huyo ni wa kimungu. Ikiwa ndivyo, linatoa mawazo fulani; linamwonyesha Mungu kuwa Mtu, na kwa hiyo linamwingiza kwenye uhusiano na watu wengine, wa kibinadamu . . . , naye anazungumza na Wazee wa Ukoo kama rafiki mmoja anavyozungumza na mwenzake.”

Kwa hiyo njia pekee ambayo mtu anaweza kumkaribia Mungu na kuwa na uhusiano wa kibinafsi naye ni kwa kumjua yeye kwa jina lake, Yahweh, au Yehova, na kwa kujifunza kutumia jina hilo kwa njia ya heshima katika kumwabudu yeye. (Yohana 17:26) Kwa hakika, wao ‘watakuja chini ya uongozi na ulinzi wake,’ maana Yehova mwenyewe anasema, “Nitamlinda kwa sababu amepata kulijua jina langu.”​—Zaburi 91:14, NW.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki