Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w82 7/15 uku. 24
  • Kinatumiwa Kuwa Kitabu cha Masomo Shuleni

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kinatumiwa Kuwa Kitabu cha Masomo Shuleni
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
w82 7/15 uku. 24

Kinatumiwa Kuwa Kitabu cha Masomo Shuleni

Habari zinazidi kutoka sehemu nyingi zikieleza namna Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia kinavyotumiwa kuwa kitabu cha masomo shuleni. Mama mmoja wa Italia anaandika hivi:

“Emanuele, mwanangu mwenye umri wa miaka minane, alipeleka nakala yake ya kitabu hiki shuleni akamwonyesha mwalimu. Mwalimu huyo wa kike alivutwa sana na habari zilizomo na kusema: ‘Nitabaki na kitabu hiki.’ Asubuhi iyo hiyo alilisomea darasa masimulizi yanayohusu yale mapigo 10 na watoto wakacheka waliposikia kwamba vyura waliingia katika nyumba za watu, hata wakafurahia kuona picha ya tukio hilo. Ndipo darasa hilo lilipopewa kazi ya nyumbani wakaandike kwa ufupi mambo waliyosika wakisomewa.

“Emanuele na mimi tulishangaa kwa sababu mwalimu anapenda sana dini yake ya Katoliki naye huwapinga Mashahidi wa Yehova. Siku chache baadaye alimwonyesha kitabu hicho padre ambaye huja kufundisha dini, akamwuliza kama ni vizuri aendelee kuwasomea watoto kwa maana kimepigwa chapa na Mashahidi wa Yehova. Padre alipofungua-fungua kitabu hicho, akasema ni kizuri sana na kinawafaa watoto kweli kweli, Akamwambia mwalimu huyo angeweza kuendelea kukitumia kusomesha watoto. Kwa hiyo, karibu kila siku mwalimu huyo huwasomea watoto hadithi moja kisha anawaambia waandike habari zinazohusu hadithi hiyo au wanaizungumza pamoja kwa mdomo.”

Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia kina masimulizi 116 ya Biblia yanayosaidia msomaji aanze kujua mambo yaliyomo katika Biblia. Kina herufi nene na picha kubwa-kubwa zaidi ya 125, na nyingi kati yazo zimechorwa kwa rangi nyingi. Unaweza kupokea kitabu hiki cha maana sana chenye kurasa 256 kwa kujaza hati ya anwani iliyo hapa na kutupelekea.

Tafadhalini nipelekeeni, mkiwa mmelipa malipo ya posta, kile Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia. Nimewapelekea ninyi shilingi 25.00 (Z30.00).

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki