Kinaweza Kubadili Maisha Yako
Kuna kitabu ambacho kwa uhakika kimebadili maisha za vijana wengi. Siku moja msichana alipeleka kitabu hicho shuleni akakisome wakati usio wa masomo. Mmoja wa wanadarasa wenzake alikuja na kumpokonya kisha akasema hivi kwa dhihaka: “Kidude gani hiki unachosoma?” Msichana huyo akamweleza kifupi yaliyomo katika kitabu Kupata Faida Zote za Ujana Wako.
Alimwonyesha mwenzake sura inayosema: “Mavazi na Sura Yako Huonyesha Ulivyo Wewe.” Mvulana mwenye kuonyeshwa alicheka na kwenda zake, lakini akakichukua kitabu chenyewe. Juma iliyofuata walikutana tena katika somo la kuhadhiriwa (kuhutubiwa) lakini sura ya mvulana huyo ikawa imebadilika sana. Alikuwa amenyoa nywele zake ndefu na akanyoa ndevu zake. Alianza kuhudhuria masomo shuleni bila kukosa hata moja. Wanadarasa wale wengine waliona badiliko kubwa lililotukia katika kijana huyo kisha wakamwomba yule Shahidi awaeleze ni kitabu gani kilichombadili sana kijana huyo. Matokeo yakawa kwamba aliwaachia vitabu vitano zaidi.
Tafadhalini mnipeleke kile kitabu chenye ngozi ngumu cha kurasa 192, Kupata Faida Zote za Ujana Wako. Mimi nimewapelekea Kshs. 6/50 (Tshs. 10/-, RWF 75). Mtanilipia bei ya kukituma kwa posta.