Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w82 12/1 uku. 24
  • Namba Moja

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Namba Moja
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
w82 12/1 uku. 24

Namba Moja

Msomaji wa Mnara wa Mlinzi aliandika hivi: “Tulipokuwa tukihudhuria Maonyesho ya Kihindi ya Choctaw huko Philadelphia, Mississippi, Julai 1981, tulipata nafasi ya kuona vitu vingi vya kupendeza kati ya sanaa na vyombo vya ufundi mwingi vya Kihindi. Tulipoviona vingine kati yavyo ambavyo vilipewa zawadi za ushindi wa kuwa bora zaidi tulishangaa kuona Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia kikiwa kimeonyeshwa kuwa namba moja kati ya vitabu vya kidini.”

Sisi tunaona kwamba hata wewe utakithamini sana kitabu hiki chenye picha za kupendeza. Maandishi yacho ni makubwa. Masimulizi ya Biblia 116 yaliyo ndani yacho yanamfahamisha msomaji mambo yanayotosha kumjulisha kwa kiasi fulani habari zilizo katika Biblia. Hadithi zilizomo zimepangwa kwa utaratibu ambao matukio yalifanyika katika historia. Utaona kwamba kitabu hiki kitakusaidia sana kujua mambo yalitokea wakati gani katika historia kuhusiana na matukio mengine. Kipokee kitabu hiki chenye thamani kubwa, cha kurasa 256, kwa kujaza hati hii yenye anwani kisha uitume.

Tafadhalini nipelekeeni Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia chenye ngozi ngumu, mkiwa mmelipia malipo ya posta. Mimi nawapelekea shilingi 25.00

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki