Kweli Yapatikana Mahali Isipoelekea Kupatikana
Barua ifuatayo kutoka kwa mwanamume katika Hartford, Connecticut, ilipokewa katika makao makuu ya Mashahidi wa Yehova:
Kwa Wo Wote Wanaohusika:
Nataka kujua kama kitabu kidogo Kweli Iongozayo kwenye Uzima wa Milele kinachapwa na Mashahidi wa Yehova. Tafadhali mniandikie na kuniambia kitabu hicho ni cha dini gani. Mimi nataka kujua kwa sababu asubuhi moja nilikuwa nikitembea katika barabara kuu ya mjini katika Hartford, nikaona kitabu hicho kidogo kimetupwa katika takataka. Ni jina la kitabu hicho lililovuta fikira zangu. . . .
Mimi ni Mkatoliki kwa sababu ndiyo dini ambayo wazazi wangu walinijulisha, lakini si kwa sababu dhamiri yangu inaniambia hivyo. Kutokana na yale ninayoweza kuona katika kitabu hicho, nasadiki kwamba nimekiona kile ambacho nimekuwa nikikitafuta kwa miaka mingi—Ile Kweli. Nami nilikipata katika lundo la takataka—Ijumaa moja 3 za asubuhi, Desemba 4, 1981. Tafadhali mnipelekee anwani ya Hartford ya kanisa la dini la kitabu hicho. Nawatakieni mwaka mpya wenye furaha,
Wasalamu,
A. C. G.
Unaweza kupokea kitabu chenye kurasa 192 Kweli Iongozayo kwenye Uzima wa Milele kwa kujaza na kupeleka kwetu hati iliyo chini.
Tafadhali mnipelekee bila malipo ya posta kitabu chenye kufungwa kwa jalada gumu Kweli Iongozayo kwenye Uzima wa Milele. Nimetia ndani Ksh 6/50, Tsh 10/-, RWF 75.