‘Kinafikia Mioyo ya Watoto’—Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
Je! wewe ungethamini kitu kinachofanya hivyo? Barua moja ya kutoka Uingereza inaeleza hivi:
“Mimi ningependa kuwajulisha kwamba kile kitabu cha rangi nyekundu-nyeupe kinachoitwa Kumsikiliza Mwalimu Mkuu kinafikia kweli kweli mioyo ya watoto wadogo. Sikuzote binti yangu anakisoma kitabu Mwalimu naye Paulo mwanangu anakisoma mara nyingi.
“Lazima niwapongeze ninyi na wafanya kazi wenu kwa sababu ya vile mmekitunga kitabu hicho. Watoto wangu wawili Paulo mwenye umri wa miaka 11 na Dawn Caroline mwenye umri wa miaka 9 1/2, wanafurahia kweli kweli vitabu vyao. Yetu ikiwa ni jamaa yenye mzazi mmoja, kitabu hicho kinanipunguzia kazi yangu kwa sababu nakala ambazo watoto wanazo zinawaongoza kwenye njia zilizonyoka.”
Wewe unaweza kuupokea msaada huo wa kulea watoto kwa kujaza na kutupelekea hati yenye anwani iliyo hapa chini, na utupelekee pia Kshs. 9.00 (Tshs. 15.00).
Tafadhalini mnipelekee kile kitabu chenye jalada gumu cha kurasa 192 kinachoitwa Kumsikilza Mwalimu Mkuu. Ninyi mtanilipia malipo ya kukipelekea kwa njia ya posta. Mimi nimewapelekea Kshs. 9.00 (Tshs. 15.00).