“Kitabu Kipya Kizuri Ajabu”
Hivyo ndivyo wasomaji wamekuwa wakisema juu ya kile kitabu kipya Unaweza Kuishi Milele katika Paradiso Duniani. Mwanamke mmoja wa Pennsylvania aliandika hivi:
“Mimi nimeshangazwa kabisa na hiki kitabu kipya kizuri ajabu . . . Picha zenyewe ni nzuri kabisa-a na rangi na michoro yacho ni mizuri sana kiasi cha kwamba inafaana na njia za kitabu hicho za kuhakikisha mambo. Na kwa kuwa mimi ni mtu aliye wa kuchunguza-chunguza hata vikosa vidogo, ni ajabu kwamba kimeweza kunivutia.”
Maoni yetu ni kwamba hata wewe utasisimuliwa na hiki kitabu kipya kizuri ajabu. Kurasa zacho 256, zenye ukubwa kama wa gazeti hili, zimejawa na picha za mafundisho zaidi ya 150, na nyingi kati yazo zina rangi za kupendeza sana. Utajua namna unavyoweza kuwa kati ya wale watakaoishi milele katika Paradiso duniani. Agiza kitabu hiki sasa. Ni cha Kshs 25/- (Tshs. 50/-, RWF 250) tu.
Tafadhalini mnipelekee Unaweza Kuishi Milele Katika Paradiso Duniani. Ninyi mtanilipia malipo ya posta. Mimi nimewapelekea Kshs. 25/- (Tshs. 50/-, RWF 250).