Kinakaza Fikira Zao Mahali Pamoja
Barua inayofuata ilipokewa na watangazaji wa gazeti hili: “Mimi ni mwalimu wa darasa la kwanza na mmoja wa wanafunzi wangu aliniletea Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia nisomee darasa langu. Hiki ndicho kitabu tu cha hadithi za Biblia ambacho kimeandikwa kwa hali na namna ya kihadithi inayoweza kuendelea kuvuta fikira za mwanafunzi wa darasa la kwanza. Hakika wamezifurahia hadithi zenyewe. . . . Mimi ninawapelekea hundi, tafadhali mnipelekee nakala moja.”
Tafadhali nipelekeeni kile kitabu chenye jalada gumu, Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia. Mimi nimewapelekea Kshs. 35.00. Ninyi mtanilipia malipo ya kukipeleka kwa posta.