Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w85 5/15 uku. 24
  • Msaada wa Kuchukuliana na Wengine

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Msaada wa Kuchukuliana na Wengine
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
w85 5/15 uku. 24

Msaada wa Kuchukuliana na Wengine

Muziki mzuri unaweza kuwa msaada huo. Mama mmoja wa Massachusetts, U.S.A., anaandika hivi: “mikazo inaelekea kuwa inaongezeka. Si kwamba nachoshwa tu na mambo ya ulimwengu, bali pia inaendelea kuwa rahisi zaidi kufikiria saa zote makosa na hali za kutokamilika za wengine kundini. Ninaanza kuzithamini tepe hizi kweli kweli​—zinaelekea kufanya akili yangu ianze tena kufikiria yanayofaa. Ningewezaje kumchukua kwa dharau ndugu au dada Mkristo wakati ninapoimba moyoni mwangu juu ya Yehova?

“Muziki mtamu nipendao zaidi ya wote ni Utepe Na. 2, Upande wa ‘A.’ Mimi nauita ‘Mwanzo wa Kifalme’​—una mwendo wa kifalme we! Binti yangu mwenye umri wa miaka sita anapenda kufungulia Utepe Na. 1, Upande wa ‘B’ ambako nyimbo laini za kupendeza zinapigwa. Hasa anapokuwa hajisikii vizuri anauomba, nasi tunaketi na kujitikisa-tikisa kitini na kuzisikiliza.”

Kila moja ya kaseti tano za muziki mtamu wa Ufalme ina bei ya Kshs. 30.00 (Tshs. 80.00, RWF 200), na kila moja inaendelea kwa karibu saa moja. Pokea kaseti zilizopangwa hapa chini kwa kujaza na kupeleka hati yenye anwani iliyopo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki