‘Watoto Wanazipenda Sana’
Mamilioni ya jamaa zimefuraha Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia. Masimulizi ya Biblia 116 yaliyomo katika kitabu hicho yanampa msomaji wazo la mambo yanayosemwa katika Biblia. Sasa kitabu hicho cha Hadithi za Biblia cha kurasa 256 kimerekodiwa katika kanda nne za kaseti kwa njia yenye kuchangamsha mioyo ya watoto. Mama mmoja wa Vancouver, British Columbia, anaandika hivi:
“Sisi tumepata furaha kama nini kwa kuwa na kanda hizo nyumbani kwetu. Tuna wasichana 2, wenye umri wa miaka 10 na 6, nao wanapenda sana kufuatana na usomaji wa hadithi hizo wakiwa wameshika vitabu vyao. Mimi pia naona huo ni msaada mkubwa katika kusaidia mtoto wangu aliye mdogo zaidi asome, kwa kuwa anaweza kuelewa mengi ya maneno yaliyo katika kitabu chenyewe. Yeye anaweza kuelewa hadithi 30 na bado hatosheki.”
Hakikisha umezipata kanda hizo za kaseti kwa ajili ya watoto wako, ikiwa bado hujafanya hivyo. Zisikilizeni hadithi hizo pamoja mkiwa jamaa. Au watoto wanaweza kujifungulia kanda hizo wakiwa pamoja na wenzao. Pakiti pamoja na kaseti nne ni Kshs. 115/- (Tshs. 300/- au RWF 750) tu, na muda zinaochukua kabla ya kumalizika ni saa 5 1/2.