Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w85 8/15 uku. 32
  • Pasta Alisahau Kwenda Kanisani

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Pasta Alisahau Kwenda Kanisani
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
w85 8/15 uku. 32

Pasta Alisahau Kwenda Kanisani

Jambo hili lililoonwa katika nchi ya Kenya linaonyesha nguvu za kuvutia za kichapo chenye mafundisho mazuri kinachoitwa Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia.

Pasta mmoja aliachiwa nakala ya kitabu hicho asubuhi moja muda mfupi tu kabla ibada haijaanza kwenye kanisa lao. Alianza papo hapo kukitazama naye akavutwa sana na yaliyomo mpaka akasahau kwenda kanisani akaongoze ibada ya kidini. Baada ya muda, wahudumu wawili wa kanisa walitumwa nyumbani kwake, wakamkuta akisoma kitabu Hadithi za Biblia. Pasta akaanza kuwaeleza namna kitabu hicho kilivyokuwa cha kusisimua sana. Wao pia wakavutwa sana nacho hata hawakurudi.

Baada ya kitambo fulani, watu wale wengine kanisani wakaenda nyumbani kwa pasta, wakashangaa kuwakuta wanaume wale watatu wakizungumza habari za Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia. Matokeo yakawa nini? Badala ya ile ibada ya kawaida kanisani asubuhi hiyo, walifanya mazungumzo ya vivi hivi juu ya kitabu Hadithi za Biblia. Wengi walitaka nakala zao wenyewe wakaomba mmisionari wa Mashahidi wa Yehova awapelekee kimoja.

Kitabu hiki chenye kurasa 256 na picha za kupendeza kinampa msomaji maelezo ya kutosha ajue ni habari gani hasa zilizo katika Biblia. Wewe unaweza kujipatia nakala yako. Jaza na upeleke hati hii yenye anwani pamoja na mchango wa Kshs. 35.00 (Tshs. 100.00 au RWF 250).

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki