Ushujaa wa Kuelekeana na Kifo
“Hivi karibuni mume wangu aliuawa na ugonjwa wa kansa,” ndivyo akaandika mwanamke mmoja wa California. “Huo ni ugonjwa unaoweza kuangamiza tumaini na hata uhai. Hata hivyo habari zilizo katika kitabu Unaweza Kuishi Milele Katika Paradiso Duniani zilisaidia mume wangu kufa akiwa na ushujaa. Kwa uhakika kinaweza kusaidia wengine waishi wakiwa na tumaini. Kila mtu anapaswa kukisoma.”
Kichapo hicho chenye kutia mtu tumaini kina kurasa 256. Ukubwa wacho ni sawa na gazeti hili, na kimejawa na picha zaidi 150, nyingi zazo zikiwa za rangi ya kupendeza sana. Jaza na upeleke hati yenye anwani iliyo hapa, pamoja na Kshs. 35.00 (Tshs. 100.00 au RWF 250), upokee nakala yako.
Tafadhali nipelekeeni, mkiwa mmelipia malipo ya posta, kile kitabu chenye jalada gumu kinachoitwa Unaweza Kuishi Milele Katika Paradiso Duniani. Mimi nimewapelekea Kshs. 35.00 (Tshs. 100.00 au RWF 250).