Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w85 9/15 uku. 32
  • Ajabu za Kumbukumbu la Akili

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ajabu za Kumbukumbu la Akili
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
w85 9/15 uku. 32

Ajabu za Kumbukumbu la Akili

Mtoto mdogo anaweza kukumbuka mambo mengi kuliko vile unavyofikiri. Katika barua ya shukrani kuhusu tepe za kaseti za Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia, mama mmoja wa Arizona anaandika hivi:

“Usiku wa leo Jamin, kivulana wangu mwenye umri wa miaka minne, ambaye bado hajui kusoma, alitajia mume wangu mambo ya hadithi kadha za Biblia karibu neno kwa neno. Amekuwa akizisikiliza kila siku kwa muda wa majuma machache. Kwa kweli, yeye anasema ni lazima afunguliwe ‘utepe wake’ ndipo apate usingizi wa mchana au alale usiku. Kabla hajaenda kulala usiku wa leo, Sid mume wangu alikuwa akimsomea Jamin hadithi ya Biblia. Mimi nikamsikia Sid akicheka kidogo. Jamin alikuwa ameimaliza hadithi ile pamoja naye. Alipojaribu nyingine kwa maneno machache tu, Jamin aliinakili yote neno kwa neno. Nikapendekeza kumjaribu katika hadithi nyingine. Jamin aliirudia-rudia hadithi hiyo. Ni wazi kwamba tulistaajabu.”

Kusikiliza kaseti za zile hadithi 116 zilizo katika Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia ni njia nzuri sana ya watoto kujifunza mambo yaliyo katika Biblia. Je! wewe unautumia msaada huo mzuri wa kufunzia? Ile pakiti yenye kaseti nne ni Kshs. 115.00 (Tshs. 320.00 au RWF 800); muda wa tepe hizo ni saa 5 1/2.

Tafadhali mnipelekee, mkiwa nimelipia malipo ya posta, ile pakiti ya hudhurungi yenye tepe nne za kaseti za Kitabu Changu Cha Hadithi za Biblia. Mimi nimewapelekea Kshs. 115.00 (Tshs. 320.00 au RWF 800).

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki