Matendo ya Fadhili Yanaleta Furaha
Mapema mwaka huu barua inayofuata ilipokewa na wachapishaji wa Mnara wa Mlinzi:
“Bwana:
“Katika Philadelphia mwezi uliopita binti yangu aliye tineja aliibiwa kibeti chake kikiwa upande wa nyuma wa mfuko wake wa vitabu. Juma lililopita alipokea katika posta kifurushi chenye kibeti chake na leseni na vipande vingine vya maana. Kifurushi hicho kilitumwa na mtu fulani aliyesema hangependa kutambulishwa, isipokuwa tu kifurushi hicho kilikuwa pia na nakala ya kichapo chenu Mnara wa Mlinzi. Inaonekana kwamba ye yote aliyefanya kitendo hicho cha upendo wa kidugu (kutoka kwenye ule mji wa upendo wa kidugu) alikipata kibeti hicho kikiwa kimetupwa na aliyekiiba kisha akajishughulisha na kujigharimisha akirudishe kwa binti yangu. Mimi na jamaa yangu tunamshukuru mtu huyo mfadhili . . . ilikuwa njia bora ya ‘kutoa ushahidi,’ hasa kwa matineja wangu (ambao ni watatu).”
Kusoma Mnara wa Mlinzi kumefaidi maisha za mamilioni ya watu, kukasitawisha ndani yao sifa za unyofu, fadhili, na kufikiria wengine. Sasa nakala zaidi ya milioni 11 za kila toleo zinachapishwa katika lugha zaidi ya 100. Unaweza kupokea andikisho la mwaka mmoja la Mnara wa Mlinzi, upokee nakala mbili kwa mwezi, kwa kujaza na kutupelekea hati yenye anwani iliyo hapa chini, pamoja na Kshs. 55.00 (Tshs. 160.00 au RWF 400).
Tafadhali nipelekeeni Mnara wa Mlinzi. Mimi nimewapelekea Kshs. 55.00 (Tshs. 160.00 au RWF 400).