Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w85 11/15 uku. 32
  • Mume Wake Alimshangaza

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mume Wake Alimshangaza
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
w85 11/15 uku. 32

Mume Wake Alimshangaza

Wakati opareta wa simu katika Texas alipotolea wafanya kazi wenzake Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia, akawaonyesha zile picha za kupendeza sana na habari zenye thamani kubwa zilizomo, wao walichukua jumla ya vitabu 50. Opareta huyo wa kike anaeleza lililotukia wakati mwanamke mmoja aliposema angependa kupata nakala.

“Nasikitika kwamba nilikuambia uniletee kitabu hicho,” akasema mwanamke huyo.

“Kwa sababu gani?” nikamuuliza.

“Sikujua wewe ni mmoja wa Mashahidi wa Yehova,” akajibu, “naye mume wangu anawachukia ninyi.”

“Pole kwamba hayo ndiyo maoni yake,” nikajibu. lakini kwa kuona kwamba mwanamke huyo alivutiwa sana na kitabu hicho, nikasema: “Tafadhali kipeleke nyumbani ukamwonyeshe, halafu asipokitaka unirudishie.”

“Haya,” akasema.

“Usiku wa kesho yake nilipokutana naye alisema, ‘JoAnn, mimi nafurahi sana. Nilikipeleka kitabu nyumbani nikakiweka juu ya meza. Nikaondoka nikanunue vyakula. Niliporudi, mume wangu alikuwa ameketi pamoja na watoto akiwasomea kitabu kile. Akaniuliza nilikipata wapi, nami nikamwambia ni kwa Mashahidi wa Yehova. Akasema, “Ni kitabu kizuri kweli kweli. Ebu zitazame picha zote hizi, tena hapa chini ya ukurasa imeonyeshwa unakoweza kupata habari zenyewe katika Biblia.” ‘ “

Sisi tunaona kwamba wewe, pia, utakifurahia kichapo hiki chenye picha za kupendeza sana na herufi kubwa-kubwa. Masimulizi yacho 116 ya Kibiblia yanampa msomaji wazo la kujua yale ambayo Biblia inasema. Hadithi hizo zimepangwa kwa kufuata utaratibu ambao matukio yalitendeka katika historia. Utaona kuwa hilo ni jambo lenye msaada katika kujifunza wakati mambo yalipotukia katika historia, kwa kuhusiana na matukio mengine. Kipokee kitabu hicho chenye thamani kubwa cha kurasa 256 kwa kujaza na kutupelekea hati yenye anwani iliyopo chini.

Tafadhali mnipelekee, mkiwa mmelipa malipo ya posta, kile kitabu chenye jalada gumu kinachoitwa Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia. Mimi nimewapelekea Kshs. 35.00 (Tshs. 100.00 au RWF 250).

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki