Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w86 6/15 uku. 32
  • ‘Ndicho Kitu Nimekuwa Nikitafuta’

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • ‘Ndicho Kitu Nimekuwa Nikitafuta’
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
w86 6/15 uku. 32

‘Ndicho Kitu Nimekuwa Nikitafuta’

Maisha za watu zinaweza kubadilishwa na jambo dogo. Hilo linaonyeshwa na msichana mdogo wa Argentina aliyeyaandikia hivi makao makuu ya ulimwengu ya Sosaiti yetu katika Brooklyn, New York:

“Mpendwa Mhariri:

Tafadhali niambie karibuni jinsi ninavyoweza kupokea gazeti Mnara wa Mlinzi mnalochapisha. Jirani yangu aliniazima nakala ya gazeti hilo na mambo niliyosoma ndani ndicho kitu ambacho nimekuwa nikitafuta kwa muda mrefu. Gazeti hilo lilinifaidi sana! Lilinipa faraja nyingi. Wajua, mimi nina umri wa miaka 15 na niko peke yangu kabisa ulimwenguni. Sina mtu wa kunihangaikia, na gazeti lenu lilinijaza tumaini. Jirani huyo aliniomba nilirudishe gazeti kwa sababu hilo ni kimoja cha vitu ambavyo mama yake, aliyekufa hivi majuzi, alimwachia.”

Msichana huyo mdogo alimalizia barua yake akieleza kwamba yeye ni maskini sana lakini angefanya yote awezayo alipie gazeti hilo. Barua yake ilipelekwa Argentina, na mwakilishi wa Sosaiti yetu akatembelea msichana huyo muda mfupi baadaye. Msichana huyo alifanya uandikisho wa Mnara wa Mlinzi na Amkeni! pia. Akafanya maendeleo ya haraka sana katika maarifa ya Biblia na kubatizwa. Sasa yeye anashiriki na maelfu ya ndugu na dada zake wa Argentina katika huduma ya Kikristo.

Wewe pia unaweza kupokea Mnara wa Mlinzi na gazeti jenzi lake Amkeni! katika sanduku lako la posta kwa kujaza na kutupelekea hati yenye anwani iliyo hapa chini.

Tafadhali mnipelekee uandikisho wa mwaka mmoja wa Mnara wa Mlinzi na Amkeni! Mimi nimewapelekea Kshs. 83.00 (Tshs. 240.00).

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki