“Kitabu cha sayansi kilicho kizuri zaidi ambacho nimepata kusoma”
Hayo ndiyo maoni ya mtu aliyekuwa mwanamageuzi kuhusu kile kitabu cha kuvutia kinachoitwa Life—How Did it Get Here? By Evolution or by Creation? Yeye anaandika hivi:
“Kwa maana mimi nilikuwa mwanafunzi wa kisayansi, nimeshangazwa sana na vile kitabu hiki kipya kimeandikwa kwa njia yenye kueleweka wazi na yenye mkazo. Nimesisimuliwa na maelezo ya kustaajabisha juu ya ulimwengu wote, yale makundi makubwa sana ya nyota, na vitu vinginevyo vyote vidogo vilivyo vigumu sana kufahamika ambavyo vinawezesha kuwe na uhai katika sayari-Dunia. Mimi nimeshangazwa na kupendezwa na zile habari zenye ubora mwingi zinazosisimua moyo kuhusu wanyama na hekima ya silika inayotuzunguka kila mahali. Tena nimenyenyekezwa na maelezo yanayohusu ubongo wa kibinadamu na mambo ya ajabu sana ambayo unaweza kufanya.
“Hata kitabu hiki kisiposaidia mtu akate shauri juu ya lile suala linalohusu mageuzi na uumbaji, mimi nafikiri ndicho kitabu kizuri zaidi cha sayansi ambacho nimepata kusoma cha kujenga uthamini wa mtu kuhusu uhai na mambo madogo madogo yaliyo magumu sana kufahamika juu ya vitu vilivyo hai. Ni kitabu cha hali ya juu sana kisayansi, hata hivyo cha kiwango kinachoweza kufahamiwa na mtu ye yote.”
Unaweza kukipokea kitabu hiki chenye picha za kupendeza cha kurasa 256 kwa kujaza na kutupelekea hati yenye anwani iliyopo chini pamoja na Kshs. 35.00 (Tshs. 100.00).
Tafadhali mnipelekee, mkiwa mmelipia malipo ya posta, kile kitabu kinachoitwa Life—How Did It Get Here? By Evolution or Creation? Mimi nimewapelekea Kshs. 35.00 (Tshs. 100.00)