Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w86 7/15 uku. 32
  • ‘Viliniinua Kutoka Hali ya Kushuka Moyo Sana’

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • ‘Viliniinua Kutoka Hali ya Kushuka Moyo Sana’
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
w86 7/15 uku. 32

‘Viliniinua Kutoka Hali ya Kushuka Moyo Sana’

Mwanamke mmoja wa Uingereza aliandika hivi:

“Bwana:

“Mwezi Februari niliagiza pakiti yenu ya kaseti za Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia, na ingawa mimi ni mtu anayepashana habari na roho za wafu, kaseti hizo zilipofika zilinivutia sana. Muda mfupi tu kabla ya hapo nilikuwa nimetoka hospitali baada ya kupata upasuaji mkubwa nami nilikuwa kitandani nikiwa nimehuzunika sana na kushuka moyo. Mume wangu aliponiletea kifurushi kile, niliamua kuzifungulia kanda hizo nizisikilize kwa kufuatana na kile kitabu.

“Hakika ziliniinua kutoka hali yangu ya kushuka moyo sana, na kwa mara ya kwanza katika muda wa siku kumi nikajisikia kikweli nikitaka kupendezwa na mazingira yangu. Wajukuu wangu wa kiume (wa miaka 6 na 8) walipokuja kunitembelea, niliwafungulia kanda hizo, nao wakafurahia sana sehemu waliokuwa na wakati wa kuisikia mpaka mimi nikawaruhusu waende nazo nyumbani wakazisikiliza zote. Kwa kuwa ni wazi kwamba wao wameona raha nyingi sana kutokana nazo, ningeshukuru kama ninyi mngeweza kunipelekea kifurushi kingine cha kanda za kaseti na kitabu ili wao waweze kubaki na zile zao.”

Mwanamke huyo aliandika nyongeza hii mwishoni mwa barua: “Katika muda wa maisha yangu nimejaribu mara nyingi kusoma Biblia yangu lakini sijapata kamwe kuifurahia wala kuielewa. Hata hivyo kanda hizi na kitabu hiki zinaieleza kwa njia yenye kueleweka wazi sana.”

Wewe, pia, unaweza kuzipokea kanda za kaseti hizi au lile buku linaloitwa Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia, au vitu vyote hivyo viwili, kwa kuijaza na kutupelekea hati yenye anwani iliyopo chini.

Tia alama katika kimoja au vyote viwili vya visanduku vinavyofuata:

[ ] Tafadhali unipelekee, mkiwa mmelipia malipo ya posta, ile pakiti ya rangi ya kahawia pamoja na zile kanda nne za kaseti za Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia, Mimi nimewapelekea Kshs. 115.00 (Tshs. 320.00)

[ ] Unipelekee lile buku la kurasa 256 linaloitwa Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia, nami nawapelekea Kshs. 35.00 (Tshs. 100.00). Tafadhali tupelekee mchango sahihi.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki