Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w86 9/15 uku. 32
  • “Mvulana Wangu Hanipi Amani Hata Dakika Moja”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Mvulana Wangu Hanipi Amani Hata Dakika Moja”
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
w86 9/15 uku. 32

“Mvulana Wangu Hanipi Amani Hata Dakika Moja”

HIVYO ndivyo baba mmoja alivyoripoti alipokuja kwenye afisi ya tawi la Sosaiti yetu katika Peru hivi majuzi. Alieleza hivi:

“Mvulana wangu mdogo amekuwa akinisumbua-sumbua kwa majuma mengi, akitaka nimnunulie kile kitabu kinachoitwa Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia. Tangu wakati mmoja wa wanashule wenzake alipokipata, mvulana wangu hanipi amani hata dakika moja. Mimi nimekuwa nikiwaza sana ni wapi ningepata nakala moja. Sikujua hata kidogo ningeanzia wapi kutafuta. Nilipouliza kwenye maduka ya vitabu sikupata matokeo.

“Nilimtajia jambo hilo mmoja wa wafanya kazi afisini kwetu, naye akaniambia niendee Mashahidi wa Yehova nikakipate. Nikasema, ‘Ah, hapana! Siendi kwa watu hao. Wao wanakuja sikuzote mlangoni pangu, nami sikuzote nawaambia waende zao.’ Lakini yeye akanisadikisha kwamba ninyi si wabaya hivyo​—kwa kweli, yeye aliwasifu sana ninyi na kusema kwamba kitabu ninachotafuta ni kizuri sana. Sasa nimekuja. Nataka kitabu hicho.”

Sisi tunaona kwamba wewe, pia, utakitaka kichapo hiki chenye picha za kupendeza sana, kilichoandikwa kwa herufi kubwa. Masimulizi yacho ya Kibiblia 116 yanampa msomaji wazo fulani ajue ni mambo gani hasa yaliyo katika Biblia.

Tafadhali mnipelekee, mkiwa mmelipia malipo ya posta, kile kichapo chenye jalada gumu kinachoitwa Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia. Mimi nimewapelekea Kshs. 35.00 (Tshs. 100.00).

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki