Mwalimu Wake Alitaka Kimoja
Hivyo ndivyo kijana mmoja alivyosema alipokipeleka kile kichapo kipya kinachoitwa Life—How Did it Get Here? By Evolution or by Creation? shuleni. Yeye anaeleza hivi:
“Nilienda shuleni nikiwa na kitabu kipya changu. Nikamwambia mwalimu wangu ningetaka kueleza darasa yaliyo katika kitabu hicho. Mwalimu huyo wa kiume alikifungua-fungua akakipenda sana hata akasimamisha darasa kufanya kazi waliyokuwa wakiendelea nayo, kisha akawaeleza yaliyomo. Kesho yake akaniuliza kama angeweza kupata kimoja. Na alasiri hiyo, baada ya shule, nikamwagushia kitabu hicho kiwe chake. Yeye anakipenda kweli kweli.”
Sisi tunaona kwamba wewe, pia, utakifurahia kitabu hiki cha kurasa 256 kinachosisimua, chenye picha za kupendeza sana. Pokea nakala yako kwa kujaza na kutupelekea hati yenye anwani iliyopo chini, pamoja na Kshs. 35.00 (Tshs. 100.00).
Tafadhali mnipelekee, mkiwa mmelipia malipo ya posta, kile kitabu kinachoitwa Life—How Did it Get Here? By Evolution or by Creation? Mimi nimewapelekea Kshs. 35.00 (Tshs. 100.00).