Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w86 10/15 uku. 32
  • Faida ya Picha Zinazofundisha

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Faida ya Picha Zinazofundisha
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
w86 10/15 uku. 32

Faida ya Picha Zinazofundisha

Mara nyingi picha zinazoonekana zinakuwa na matokeo makubwa katika kufundisha mawazo ya maana kuliko maneno yaliyoandikwa. Mama mmoja anaeleza jinsi alivyofarijiwa na picha moja:

“Picha zenye mafaa zilizo katika kitabu Unaweza Kuishi Milele Katika Paradiso Duniani ndizo nimekuwa nikipenda zaidi ya mambo mengine kwa sababu zinaelekeza fikira wazi-wazi na bila kukawia katika jambo linalozungumzwa.

“Lakini, uthamini wangu kwa uwezo wa kufundisha wa picha hizo uliongezeka sana Jumapili iliyopita wakati mshiriki wa jamaa yetu alipopatwa na aksidenti. Mwana wetu aliye mdogo, Aaron, alivunja mkono, na daktari akaeleza kwamba ilikuwa lazima apasuliwe ili mkono urudishwe kama ulivyokuwa. Wakati mwana wetu alipokuwa akisukumwa katika kile kitanda chenye magurudumu, nilijisikia nikifadhaika sana moyoni. Wakati ulipoendelea sana, hangaiko langu likaongezeka.

“Halafu nikaikumbuka ile picha iliyo katika sura ya 11, katika ukurasa 100. Maana kuu ya maneno yaliyoandikwa chini ya picha hiyo ni kwamba, ‘Kama vile mzazi anavyoruhusu mtoto apate upasuaji wenye maumivu, Mungu pia ana sababu nzuri za kuruhusu kwa muda wanadamu wataabike.’ Niliporudisha wazo hilo akilini tena na tena, amani ya Mungu ilitua juu yangu, nami nikaweza kudumisha utulivu wangu wa kujiweza.

Kichapo hicho kizuri sana kina picha 150 za mafundisho zilizo nzuri kabisa, na nyingi kati yazo zina rangi ya kupendeza sana. Jaza na utupelekee hati yenye anwani iliyo hapa chini, pamoja na Kshs. 35.00 (Tshs. 100.00). Utapokea nakala yako.

Tafadhali mnipelekee, mkiwa mmelipia malipo ya posta, kile kitabu chenye jalada gumu cha kurasa 256 kinachoitwa Unaweza Kuishi Milele Katika Paradiso Duniani. Mimi nimewapelekea Kshs. 35.00 (Tshs. 100.00).

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki