Ungamo la Myesuiti
WATU wengi leo wanaamini kwamba Desemba 25 ni siku takatifu, siku ya kuzaliwa kwa Yesu. Walakini, uhakika wa kwamba umaana wa kweli wa kidini wa siku umejulikana kwa muda mrefu na viongozi wa kidini unaonyeshwa na maneno yafuatayo kutoka kitabu cha Urbanus Holzmeister, mwanachuo Myesuiti:
“Leo imekubaliwa na watu wote kwamba pindi ya sherehe ya siku ya Desemba 25 ilikuwa sikukuu ambayo wapagani walisherehekea siku hii. Tayari Petavius [mwanachuo Mfaransa Myesuiti, 1583-1652] ameeleza kwa usahihi kwamba ‘sikukuu ya jua lisiloshindwa lilisherehekewa katika Desemba 25.’
“Mashahidi wa sikukuu hii ni: (a) Kalenda ya Furius Dionysius Filocalus, iliyotungwa mwaka 354 [W.K.], ambamo imesemwa kwamba: ‘Desemba 25, S(ikukuu) ya (Jua) lisiloshindwa.’ (b) kalenda ya mnajimu Antiochus (iliyotungwa karibu 200 [W.K.]): ‘Mwezi wa Desemba . . . 25 . . . Siku ya kuzaliwa kwa Jua; mchana unaongezeka.’ (c) Caesar Julian [Julian Mwasi-lmani, mfalme wa Roma, 361-363 W.K.) alipendekeza michezo iliyosherehekewa mwishoni mwa mwaka kwa kuheshimu jua, lililoitwa ‘jua lisiloshindwa.’”—Chronologia vitae Christi [Tarehe ya Maisha ya Kristo], Pontificium Institutum Biblicum, Rome, 1933, ukurasa 46.