‘Kitu Kizuri Sana kwa Bei Ndogo Sana’
Ndivyo anavyohisi mama mmoja kutoka Pennsylvania U.S.A., kuhusu kaseti zilizorekodiwa za Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia. Anaandika hivi:
“Nina wana wawili Steven (mwenye miaka 9) na Robert (mwenye miaka 4). Kila mara Robert anamwuliza Steven amsomee Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia. Nilikuwa nikifikiria kuziingiza hadithi kwenye kanda mimi mwenyewe lakini sijapata wakati wa kutosha kufanya hivyo. Nashukuru kwa msaada wenu sasa, kwa kuwa naweza kuzinunua kanda zilizorekodiwa kwa karibu kiasi kile ambacho kanda tupu zinagharimu. Ni vizuri sana kujua kwamba tungali tunaweza kununua kitu kizuri sana, kwa mtu anayethaminiwa sana, kwa bei ndogo sana.”
Ikiwa hujafanya hivyo ‘bado, hakikisha unawanunulia watoto wako kanda hizi. Zisikilizeni hadithi pamoja mkiwa jamaa. Au watoto wanaweza kuzipiga kanda hizo wakiwa peke yao au pamoja na marafiki wao. Zile kaseti nne, kutia pakiti ambamo zinakuwa ni Kshs. 115.00 (Tshs. 320.00) zinachukua saa: 5 1/2. Kitabu Hadithi za Biblia chenye kurasa 256, na picha zenye kupendeza ni Kshs. 35.00 (Tshs. 100.00).
Tafadhali onyesha kwa kutia alama katika visanduku hivi mbalimbali uonyeshe kama unataka kitabu chenyewe au ile pakiti ya kanda za kaseti, au vyote viwili.
◻ Mimi nimewapelekea Kshs. 35.00 (Tshs. 100.00) kwa ajili ya Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia.
◻ Mimi mmewapelekea Kshs. 115.00 (Tshs. 320.00) kwa ajili ya ile pakiti ya rangi ya hudhurungi yenye kanda za kaseti nne za Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia.