Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w87 10/15 uku. 32
  • Binti Aliikosa Basi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Binti Aliikosa Basi
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
w87 10/15 uku. 32

Binti Aliikosa Basi

SIKU moja James aliona Rebeka binti yake akitembea kwa upole-pole usio wa kawaida kwenda kuikuta basi ya shule. Ingawa Rebeka angeweza kuiona basi ikija, yeye alitembea pole pole hata zaidi na kwa makusudi akaikosa basi.

Jioni iyo hiyo James na mke wake, Veronica walizungumza jambo lile kwa kurudia ile hadithi ya “Yona na Samaki Mkubwa” kutoka Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia. Ilikuwa moja ya hadithi ambazo Rebeka anapenda sana. Baada ya kumaliza hadithi ile, wazazi waliihusianisha na tatizo la binti yao. Yeye kwa kweli alielewa maana na kusema: “Hata ingawa Yona alikimbia na kuingia ndani ya matata katika bahari, na yeye alimezwa na yule samaki na kutapikwa nje​—kazi yake kwa Yehova ilikuwa bado inamngoja aifanye.”

Siku iliyofuata, Rebeka alienda shuleni akiwa na mwelekeo mpya na Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia kikiwa katika kwapa la mkono wake.

Wewe unaweza kupokea nakala ya kichapo hiki cha kurasa 256 chenye picha za kupendeza na herufi kubwa kwa kujaza na kutupelekea hati yenye anwani iliyopo chini.

Tafadhali mnipelekee, mkiwa mmelipia malipo ya posta, kile kitabu chenye jalada gumu kinachoitwa Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia. Mimi ninawapelekea ninyi Kshs. 40/- (Tshs. 110/-).

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki