Kutazama Ugiriki
Wakaaji wa Ugiriki wanaojulikana kuwa ndio wa mapema zaidi kuwa huko waliitwa Waionia. Inaitikadiwa kwamba jina hilo lilitokana na Yavani (Kiebrania, Yawan’) mzee wa ukoo wao, ambaye alikuwa mwana wa Yafethi na kwa hiyo alikuwa mjukuu wa Noa. (Mwanzo 10:1, 2) Katika Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo ya Biblia, Ugiriki inaitwa Hellas’. Hilo ni bara lenye miinuko-miinuko na lenye miamba-miamba, likiwa na milima yenye misitu iliyoshikana sana. Zamani za kale Wagiriki walikuja kuwa mabaharia stadi.
Wagiriki wa kale walikuwa na miungu mingi, iliyosimuliwa kuwa yenye umbo la kibinadamu lenye uzuri mwingi wa kuvutia. Miungu hiyo inadhaniwa kuwa ilikula, ikanywa, na kulala; na ingawa ilifikiriwa kuwa mitakatifu na isiyoweza kufa, hiyo ilitongoza na kunajisi pia na ilikuwa na uwezo wa kudanganya na kufanya uhalifu. Hadithi hizo za ubuni huenda kwa kweli zikawa ni kumbukumbu zilizopotoshwa za wakati uliokuwa kabla ya Gharika wakati wana wa kimalaika wa Mungu walipokuja duniani kwa uasi, wakaingiliana na wanawake, wakazaa wazao wenye nguvu nyingi walioitwa Wanefili, na kujaza dunia jeuri.—Mwanzo 6:1-8, 13.
Katika karne ya nne K.W K, Filipo wa Makedonia, baba ya Aleksanda Mkuu, alijiondokea kwenda kuungamanisha mikoa-majiji ya Kigiriki ambayo hapo kwanza ilikuwa ikijitegemea yenyewe, akaileta chini ya udhibiti wa Kimakedonia. Katika karne ya pili K.W.K., Ugiriki ikawa mkoa wa Kiroma, na utamaduni wa Kigiriki ukaenea kufika Roma.
Kutumiwa kotekote kwa Kigiriki cha koi·neʹ kulichangia mpanuko wa haraka sana wa habari njema za Kikristo katika sehemu zote za eneo la Mediterania.
Mtume Paulo alizuru Makedonia na Ugiriki wakati wa talii zake za umisionari za pili na tatu Yeye alifanyiza makundi ya Kikristo katika Filipi, Thesalonike, Korintho, na Beroya. Sila, Timotheo, Tito, na Wakristo wengine wa mapema walifundisha huko pia. Leo, Ugiriki ina makundi zaidi ya 320 ya Mashahidi wa Yehova na watangazaji wanaozidi 23,000 wa Ufalme wa Mungu.