Kukabiliana na Magumu ya Maisha
Mwaka jana nyumba ya mwalimu mmoja katika Bignona, Senegali, iliteketea kabisa. Baadaye tawi la Sosaiti ya Mnara wa Mlinzi katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi lilipokea barua hii:
“Jambo linaloniudhi mimi sana,” mwalimu huyo akaeleza, “ni kwamba katika moto huo nilipoteza vitabu ambavyo kwangu ni vya thamani kubwa isiyoweza kukadiriwa. Vichwa vya vitabu hivyo ni kutia ndani Kupata Faida Zote za Ujana Wako na Je! Uzima Ndio Uu Huu Tu? Mimi naweza kuendelea na maisha bila nguo zangu na nyumba yangu, lakini siwezi kuendelea nayo bila vitabu hivyo! Hivyo ni vya maana kwangu kuliko vitu vinginevyo vyote ambavyo nilipoteza. Mimi nawaomba ninyi, tafadhali mnipashe habari upesi iwezekanavyo, na kunijulisha jinsi ninavyoweza kupata nakala za kuwa mahali pa zile nyingine. Maisha yamejaa magumu, nasi tunahitaji habari kama hizo ili kuyatatua na kutusaidia tufanye maamuzi yanayofaa na kujiendesha wenyewe ifaavyo.”
Wengine wengi wanahisi hivyo hivyo juu ya vichapo hivyo viwili. Kwa uhakika, nakala zaidi ya milioni 22 za kitabu Ujana na nakala zaidi ya milioni 20 za Je! Uzima Ndio Uu Huu Tu? Zimegawanywa ulimwenguni pote. Wewe unaweza kupokea vitabu hivyo viwili vilivyo muhimu kwa kujaza na kutupelekea tu hati yenye anwani iliyopo chini, pamoja na mchango wa Kshs. 30.00 (Tshs. 160.00)
Tafadhali mnipelekee, mkiwa mmelipia malipo ya posta, vile vitabu viwili vya kurasa 192 vyenye jalada gumu, Kupata Faida Zote za Ujana Wako na Je! Uzima Ndio Uu Huu Tu? Mimi nawapelekea Kshs. 30.00 (Tshs. 160.00).