Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
Mamilioni ya jamaa zimefurahia Kumsikiliza Mwalimu Mkuu, kitabu kilichotungwa kwa njia ya kusomwa na watoto. Hadithi zacho 46 za Biblia husisimua watoto, zikiwafundisha pia viwango bora vya kiadili. Sasa kitabu hicho chenye thamani kubwa kilicho na kurasa 192 kimerekodiwa . . . katika kanda za kaseti nne. Mnaweza kusikiliza hadithi hizo pamoja mkiwa jamaa nzima. Au watoto wanaweza kufungulia kanda hizo kwa ajili yao wenyewe na waandamani wao. Pakiti ile yenye kaseti nne na kitabu Kumsikiliza Mwalimu Mkuu ni Kshs. 160.00 (Tshs. 800.00) tu. Urefu wa wakati wazo unazidi kidogo saa 5. Sasa Katika Kaseti Nne Katika Pakiti Moja ya Mkononi
Tafadhali mnipelekee, mkiwa mmelipia malipo ya posta, ile pakiti ya rangi nzuri ya kahawia iliyo na kanda za kaseti nne na kitabu Kumsikiliza Mwalimu Mkuu. Mimi nawapelekea Kshs. 160.00 (Tshs. 800.00).