Hadithi Ambazo Watoto Wanapenda
WAKA uliopita makao makuu ya Sosaiti ya Mnara wa Mlinzi katika Brooklyn yalipokea barua inayofuata kutoka Sherwood, Oregon:
“Mabwana:
“Hivi majuzi nilichukua kwenye maktaba kitabu chenye kichwa Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia kwa ajili watoto wangu wa miaka 4 na 6. Hadithi zenyewe zimesimuliwa kwa njia wanayoweza kuelewa vizuri, nao wameona shangwe kamili ya kusoma hadithi hizo za Biblia. Sisi tungependa kuongezea kitabu hicho kwenye maktaba yetu ya kibinafsi.
“Nyuma ya kitabu hicho inasemwa kwamba nakala ingeweza kupatikana kwa kuandikia anwani hii na kupeleka dola 2.00. Kitabu hicho kinaonekana ni kama kimekuwa kikichapwa kwa muda fulani. Je! “mnaweza kuniambia gharama ya sasa ili nipeleke malipo na kupokea kitabu chenyewe?”
Kilipotolewa katika 1978 (1981 katika Kiswahili), Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia kilikuwa Kshs. 25.00 (dola 2.00), lakini sasa mchango ni Kshs. 40.00 (Tshs. 200.00). Wewe pia ungeweza kupokea nakala ya kichapo hiki cha kurasa 256, chenye vielezi vya kupendeza na herufi kubwa, kwa kujaza na kutupelekea hati yenye anwani iliyopo chini pamoja na Kshs. 40.00 (Tshs. 200.00).
Tafadhali mnipelekee, mkiwa mmelipia malipo ya posta, kile kitabu chenye jalada gumu Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia. Mimi nimewapelekea Kshs. 40.00 (Tshs. 200.00).