Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w89 2/1 uku. 32
  • Mahali Alikotoka Ibilisi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mahali Alikotoka Ibilisi
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
w89 2/1 uku. 32

Mahali Alikotoka Ibilisi

“Kazi zangu hasa ni kufanya watoto wabaki wakiwa wamefungwa katika mishipi ya viti vyao na kuwafanya wakae kimya,” ndivyo anavyoeleza kijana mmoja mwanamke anayefanya kazi ya nusu-siku akiwa msimamizi wa watoto katika basi ya shule katika Dakota ya Kusini. Yeye anasimulia hivi:

“Mmoja wa wavulana wale hunitatiza sana. Kumbuka, yeye ni wa miaka sita tu, hata hivyo nyakati nyingine kinywa chake kinaweza kufanya baharia abadilike rangi ya uso kwa aibu nyingi. Mimi nimelazimika kumketisha katika kiti chake kwa ujasiri na kuketi nikiwa nimemziba kinywa kwa mkono wangu ili akae kimya. Yeye amewahi kunipiga mateke, kunikwaruza-kwaruza kwa kucha zake, kunichuna, kunilaani-laani, na kupiga makelele mengi. Siku fulani ikiwa mbaya, kunakuwa na uhitaji wa kumkalia.

“Ijumaa ilikuwa siku mbaya, na karibu wakati ule ambapo mimi nilikuwa nimechoka mwili wote tangu mabegani, yeye aliuliza: ‘Kwa nini Mungu alimfanyiza Ibilisi?’ Kulikuwa na nakala ya Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia katika basi hiyo. Mimi nikamwambia kwamba kitabu hiki kingemsaidia aone mahali alikotoka Ibilisi. Je! ungeitikadi ya kwamba sisi tumepitia hadithi 41 tukiwa pamoja? Mimi nilikuwa karibu kumchoka mtoto huyo, lakini mwelekeo wake umebadilika kufikia hatua ya kwamba yeye hataki kuondoka kwenye basi hiyo tufikapo shuleni. Yeye hutaka tuzidi kuzungumza juu ya hadithi nyinginezo!”

Kujifunza kichapo hicho cha kusifika kumeleta matokeo yanayofanana na hilo kuhusiana na watoto wengine wengi. Wewe unaweza kupokea nakala moja ya kichapo hiki chenye vielezi vizuri na chapa kubwa, cha kurasa 256, kwa kujaza na kutupelekea hati yenye anwani iliyopo chini, pamoja na Kshs. 40/= (Tshs 200/=; RWF 250).

Tafadhali mnipelekee, mkiwa mmelipia malipo ya posta, kile kitabu chenye jalada gumu

Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia, Mimi nimewapelekea nyinyi Kshs. 40 (Tshs. 200/=; RWF 250).

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki