Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w89 2/15 uku. 32
  • ‘Hawajawa na Furaha Ile Waliyo Nayo Sasa’

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • ‘Hawajawa na Furaha Ile Waliyo Nayo Sasa’
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
w89 2/15 uku. 32

‘Hawajawa na Furaha Ile Waliyo Nayo Sasa’

Hilo lilikuwa elezo la mwanamke aliyekuwa ametumia ushauri ulioandaliwa katika kitabu Kufanya Maisha ya Jamaa Yako Yawe Yenye Furaha. Alikuwa na matatizo ya ndoa na akaanza kuyazungumzia pamoja na mwanamke mwenye kusafisha nyumba yake. Bibi msafishaji aandika hivi:

“Ushauri wowote niliompa ulitoka mle mle kitabuni. Hatimaye nilimwambia nilikuwa na kitabu ambacho kingeweza kumpendeza. Nikaeleza kilivyokuwa kimenisaidia mimi na kwamba kilikuwa na mambo mengi ya kiakili kutokana na Biblia. Siku chache baadaye, nilinena naye katika simu nikajulishwa kwamba yeye na mume wake walikuwa wamekisoma na kuamua kutendeana vizuri kidogo.

“Jioni hii mwanamke huyo alinipigia simu tena aniambie, miongoni mwa mambo mengineyo, kwamba maisha yao hayajawa na furaha ile yaliyo nayo sasa. Wamekisoma kitabu pamoja, wakakichunguza katika Biblia, na wanatumia kanuni zilizomo.”

Ikiwa wewe unatamani msaada kufanya ndoa yako iwe yenye furaha zaidi, unaweza kunufaika na kitabu hiki. Pokea nakala kwa kujaza na kutupelekea hati yenye anwani iliyopo chini.

Tafadhali mnipelekee, mkiwa mmelipia malipo ya posta, kile kitabu cha kurasa 192,

Kufanya Maisha ya Jamaa Yako Yawe Yenye Furaha. Mimi nawapelekea Kshs. 15/-.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki