Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w89 5/1 uku. 32
  • Chombo Chenye Thamani Kubwa kwa Utafiti

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Chombo Chenye Thamani Kubwa kwa Utafiti
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
w89 5/1 uku. 32

Chombo Chenye Thamani Kubwa kwa Utafiti

Asanteni kwa vichapo vyenu vya mabuku ya Mnara wa Mlinzi na Amkeni!,” anaandika msichana wa miaka 13 kutoka New Zealand. Anaeleza hivi:

“Mwalimu wangu aliomba darasa lifanye utafiti juu ya msiba wowote kisha wauandike kwa namna ya kijitabu. Mimi nikachagua kuchunguza habari za Titanic. Nilitafuta vitabu shuleni nisipate chochote kilichofaa. Basi nikatazama katika buku la Amkeni! ya ’81. Niliisoma makala nzima juu ya Titanic, halafu kwa maneno yangu mwenyewe, nikaiandika kwa namna ya kijitabu. Mwalimu alipokwisha kutia maksi katika migawo yote, alionyesha darasa mgawo wangu. Mimi nilipata maksi za juu kupita zote.” Kijana huyo anamalizia hivi: “Nikiwa na mgawo wakati wowote, nitatumia vichapo vyenu.”

Kwa kujipatia mabuku yaliyojalidiwa ya jarida hili, wewe pia utakuwa na chombo chenye thamani kubwa kwa utafiti. Sasa buku lililojalidiwa la Amkeni! za 1988 linapatikana (kwa Kiingereza), na pia buku lililojalidiwa la Mnara wa Mlinzi, gazeti andamani la Amkeni! Pokea mabuku yako kwa kujaza na kutupelekea hati yenye anwani iliyopo chini.

Tia alama kisanduku kimoja au vyote viwili, na utupelekee mchango sahihi.

[ ] Tafadhali mnipelekee buku lililojalidiwa la Amkeni! za 1988 (kwa Kiingereza). Mimi nawapelekea Kshs. 96.00 (Tshs. 480.00; RWF 600)

[ ] Tafadhali mnipelekee buku lililojalidiwa la Mnara wa Mlinzi wa 1988 (kwa Kiingereza). Mimi nawapelekea Kshs. 96.00.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki