Yanaufikia Moyo
Mama mmoja kutoka Virginia, U.S.A. anaandika hivi: “Sisi tuna mwana wa miaka mitano, Keith. Kwenye hatua hii ya maisha yake, akili yake haifikirii mambo ya dini hasa. Hii si kusema kwamba yeye si mvulana mwema. Ni mwenye upendo sana na mfadhili na husikiliza dhamiri yake. Lakini kwa kawaida yeye hupuuza tunapojaribu mara nyingi kufanya naye mazungumzo ya Biblia, au hubadili haraka kichwa cha mazungumzo. Kwa hiyo sisi husali kuomba saburi na kutafuta njia nyingine za kukaza kikiki kweli za kiroho ndani ya moyo wake mchanga.
“Sasa mvulana huyu amekuza upendezi wa kusisimukia hadithi. Tumia kitabu cha Hadithi za Biblia halafu zile kanda. Nyanya yake alimpa mashine ya kaseti. Sisi tukamwonyesha jinsi ya kuitumia. Sasa yeye huketi saa nyingi kwa wakati mmoja, kitabu chake kikiwa mkononi, akifuatisha pamoja na kanda zile.
“Kwa desturi wakati wa kulala hapa ni wakati wa hadithi. Usiku wa leo nilisema nimechoka mno, lakini labda yeye angeweza kunisimulia moja. Niliomba hadithi moja ya Biblia. Ebu wazia nilivyofurahi alipoanza kuniambia juu ya Ayubu, halafu Daudi na Goliathi, halafu Ruthu na Naomi. Alipofika kwenye sehemu ile ambapo Ruthu anakuja kumpenda sana Yehova, alicheka-cheka akasema, ‘Hiyo ndiyo sehemu niipendayo zaidi!’
“Baraka zaidi ilikuja nilipotambua kwamba yeye huiga pia kuinua na kushusha sauti katika silabi zinazofaa za maneno, kutua penye alama za vituo, na anazoea uchaguzi bora wa maneno! Naye hurudia kusimulia hadithi hizi neno kwa neno! Asanteni, asanteni, asanteni!”
Kweli kweli, mtoto mchanga anaweza kukumbuka mengi kuliko vile wewe unavyofikiri akiwa na upendezi wa kufanya hivyo. Jamaa nyingi zimepata kwamba Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia, pamoja na kurekodiwa kwa kitabu hicho katika kanda za kaseti, ndicho kitu kinachohitajiwa hasa ili kuamsha upendezi huo. Wewe unaweza kupokea hizo kanda za kaseti au lile buku Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia, au vyote viwili, kwa kujaza na kutupelekea hati yenye anwani iliyopo chini.
Tia alama katika moja au sehemu zote mbili zinazofuata, na ulipe mchango ulio sahihi:
[ ] Tafadhali mnipelekee, mkiwa mmelipia malipo ya posta, ile pakiti kahawia ya vainili pamoja na kanda za kaseti nne za Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia. Mimi nawapelekea Kshs. 150/=
[ ] Tafadhali mnipelekee kile kitabu cha kurasa 256 chenye picha, Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia, ambacho ili nikipate nawapelekea Kshs. 40/=