“Kumbe Mungu Niliyekuwa Nimekuwa Nikimtafuta Ndiye Huyo Hapa”
Wapi? Mtu huyo alikuwa akiongea juu ya nini?
Hadithi hiyo inarudi nyuma kwenye wakati ambapo zawadi ya kitabu Life —How Did It Get Here? By Evolution or by Creation? ilitolewa. Kitabu hicho kilitolewa kwa mhadhiri wa vitu vya kale aliyestaafu anayeishi Hispania. Baadaye, mtu yule aliyekuwa ameitoa zawadi ile alipozuru Hispania, mhadhiri huyu aliyestaafu alionelea hivi: “Na kabla sijasahau, Edwin, asante kwa kupeleka kitabu kile. Nilikisoma lakini nikampa kivulana Mhispania.”
Kijana huyo Mhispania alikuwa akitumia dawa za kulevya, akiwa na ndevu nyingi na nywele ndefu. Hata hivyo, baada ya mwanamume huyo kijana kupokea kitabu kile, mgeuzo wenye kutazamisha ulitokea katika kivulana yule. Alinyoa ndevu zake, akakata nywele zake, na akaacha kutumia dawa za kulevya. Alipopata kujua hilo, Edwin alikuwa na hamu ya kukutana naye.
Walipokutana na kijana huyo mdogo akapata kujua kilikotoka kitabu kile, alimkumbatia Edwin na kusema: “Kwa miaka mitano mimi nimekuwa nikimtafuta Mungu, na nilipofungua kitabu kile, kumbe Mungu niliyekuwa nimekuwa nikimtafuta ndiye huyo hapa.” Kivulana huyo alikuwa amefanya maendeleo kufikia hatua ya kushiriki na wengine imani yake mpya.
Sisi tunahisi kwamba wewe pia utanufaika na kitabu hiki kizuri sana ambacho kimeathiri maisha za watu kwa njia yenye kunufaisha. Unaweza kupokea nakala ya kichapo hiki kilichofanyiwa utafiti kamili kwa kujaza na kutupelekea hati yenye anwani iliyopo chini.
Tafadhali pelekeni, mkiwa mmelipia malipo ya posta, kile kitabu chenye kurasa 256 chenye jalada gumu, Life—How Did It Get Here? By Evolution or by Creation? Mimi nawapelekea nyinyi Kshs. 50/- (Tshs. 360/-).