Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w90 1/1 uku. 15
  • Mnyanyaso Waendelea Katika Burundi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mnyanyaso Waendelea Katika Burundi
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
w90 1/1 uku. 15

Mnyanyaso Waendelea Katika Burundi

MAPEMA katika 1989, watawala wa lile taifa la Afrika ya kati la Burundi walifungulia wimbi la mnyanyaso juu ya Mashahidi wa Yehova. Kama ilivyoripotiwa katika toleo la Agosti 15, 1989 la Mnara wa Mlinzi,. wenye mamlaka walijaribu kulazimisha Mashahidi waache imani yao, wakitumia vitendo vya kuwasumbua-sumbua, kuwakamata-kamata, kuwapiga-piga, na hatua nyingine za kuwatenda vikali. Hali imekuwa nini tangu wakati huo?

Ripoti nyingine kutoka Burundi yasema kwamba wakati mwangalizi wa wilaya alipozuru Kinyinya na Gitega, wenye mamlaka walijaribu kukamata washirika wa kundi kwenye mkutano mmoja. Waangalizi wa wilaya na mzunguko waliweza kuponyoka, lakini wale waliokamatwa walikuwa ni kutia ndani wanafunzi wawili wa shule ya sekondari na msichana mmoja katika shule ya msingi. Wote walipigwa. Siku iliyofuata Mashahidi waliokamatwa waliletwa mbele ya gavana wakaeleza kwa nini hawangeweza kuwa washirika wa chama cha kisiasa. Walipigwa tena. Ripoti nyingine zaeleza juu ya matukio kama hayo.

Mzee mmoja Mkristo mwenye daraka katika Burundi aandika: “Hakuna Shahidi wa Yehova ambaye amekamatwa kwa wizi, uuaji, au kufitini serikali. Ikiwa wenye mamlaka wana misingi halisi ya kuadhibu Mashahidi, acheni wafanye hivyo katika mahakama ya peupe badala ya kutesa-tesa raia wenye kutafuta amani, huku wakitwaa mali zao kinguvu, na kuwafukuza kama wanyama-mwitu. Ndugu wengi katika maeneo ya ndani-ndani wameshurutika kukimbia nyumba zao na kuishi kama watoro. Dada mmoja ambaye mume wake yumo gerezani ameenda kuona wenye mamlaka wengi kwa jitihada ya kufanya mume wake aachiliwe. Wote hao wamemwambia aende zake kwa kumpa jibu hili: ‘Sisi hatuwezi kamwe kuachilia mume wako na huku wewe wapokea pesa kutoka ng’ambo ili uvuruge uthabiti wa nchi yetu.’ Uchongezi gani huo!”

Hata hivyo, kuna habari njema kutoka Burundi. Mashahidi wa huko hawajikunji kwa woga wala kutishika. Kuhubiri habari njema kwapanuka kwa busara lakini kwa uhakika, na akina ndugu na dada wang’amua kwamba waweza kuvumilia kwa tegemeo kamili katika Yehova. Tayari barua nyingi za kuonyesha uchukizo kwa mambo yanayotendwa zimeandikwa zikapelekwa Burundi, na bila shaka nyingine nyingi zaidi zitafuata wakati ulimwengu utakapong’amua kwamba Burundi inaendelea na kampeni yayo isiyo na rehema ya mnyanyaso dhidi ya Mashahidi wa Yehova.

[Sanduku katika ukurasa wa 15]

Anwani ya rais wa Burundi ni hii:

His Excellency Major Pierre Buyoya

President of the Republic of Burundi

Bujumbura

REPUBLIC OF BURUNDI

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki