“Hakizunguki-zunguki kwa Kukosa Shabaha”
Kukua katika nyakati hizi zenye matata si rahisi. Vijana hukabili hali mpya nyingi na kulazimika kufanya maamuzi mengi mazito. Je! ninywe pombe? Nikubali dawa za kulevya? Ni mwenendo gani ambao yafaa kuwa nao pamoja na jinsia tofauti? Vijana wahitaji majibu yenye matokeo, yasiyozunguka-zunguka kwa kukosa shabaha. Aliposoma kile kitabu kipya Questions Young People Ask—Answers That Work, kijana mmoja wa Greensboro, Carolina ya Kaskazini, aliandika hivi:
“Kitabu hiki chaeleza mambo mengi sana na kina vielelezo vizuri kwa kila tatizo. Ukiisha kuanza kukisoma, huwezi kamwe kukiweka chini, sura zenyewe ni za kupendeza sana. Hakizunguki-zunguki kwa kukosa shabaha, bali hutoa majibu ya moja kwa moja ya tatizo.
“Kwa ujumla, kitabu hiki ni kizuri ajabu, cha kweli kabisa, cha kuvutia sana, . . . maneno hayawezi kabisa kuonyesha jinsi kitabu hiki kilivyo kizuri. Mimi ningependekeza sana kitabu hiki kwa watu wote, hususa vijana.”
Pokea sasa kitabu kipya hiki chenye kuvutia kwa kujaza na kutupelekea hati hii yenye anwani. Ni Kshs. 20/= (Tshs. 120/=) tu.
Tafadhali mnipelekee kile kitabu chenye kurasa 320 na jalada gumu, Questions Young People Ask—Answers That Work. Mimi nawapelekea Kshs. 20/= (Tshs. 120/=; RWF 100).