“Njia Nzuri Ajabu ya Kufundisha”
Hivyo ndivyo mtu mmoja kutoka Springfield, Oregon, U.S.A., alivyosema kuhusu kanda za kaseti za kitabu Kumsikiliza Mwalimu Mkuu (kwa Kiingereza). “Hii ni njia nzuri ajabu ya kufundisha mtu yeyote,” ndivyo mwanamke huyo aandika. “Ushauri ule timamu kwa wazazi na watoto umetolewa kwa njia nzuri sana! Niwezalo kusema tu ni kwamba njia ambayo kitabu hiki kimesomwa na hadithi zikasimuliwa ni ‘nzuri ajabu’! Sisi twawatolea asante za mioyo mikunjufu kabisa! Tafadhali mtupelekee seti mbili zaidi. Tumeambatanisha cheki kwa ajili ya kanda hizo.”
Pakiti hiyo ina kanda za kaseti nne na kitabu Kumsikiliza Mwalimu Mkuu (kwa Kiingereza). Urefu wa muda wazo unazidi kidogo saa tano. Kitabu hicho kimekusudiwa kwa kusoma pamoja na wachanga, lakini familia nzima yaweza kunufaika kwa kusikiliza kanda hizo ikiwa pamoja. Au watoto waweza kufungulia kanda hizo ili wasikilize wao wenyewe na waandamani wao.
Hii ni sehemu ya kazi ya elimu ya Biblia ulimwenguni pote ambayo hutegemezwa na michango ya kujitolea kwa hiari.
Mimi ningependa kupokea ile pakiti ya plastiki pamoja na kanda za kaseti nne na kitabu Kumsikiliza Mwalimu Mkuu (kwa Kiingereza).