Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w90 8/15 uku. 32
  • Naweza Kukabilianaje na Msongo wa Marika

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Naweza Kukabilianaje na Msongo wa Marika
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
w90 8/15 uku. 32

Naweza Kukabilianaje na Msongo wa Marika

Barua moja kutoka kwa ofisa wa polisi mmoja wa Chicago yatoa kielezi cha umaana wa kujua jibu hilo. Aandika hivi:

“Mnamo Januari 15, 1990, nilikuwa nikishughulikia mfungwa wa miaka 18 aliyerudishwa Chicago kutoka Mississippi nikiwa na waranti ya mtorokaji. Sehemu ya shughuli hiyo ni kutwaa mali yote ya mfungwa. Kati ya mali zake kulikuwako kitabu Young People Ask.

“‘Je! ulisoma kitabu hiki?’ nikauliza.

“‘Ndiyo,’ akajibu, ‘nilipokuwa nimejificha kule Mississippi, nilifanya kazi kwenye shamba, na wawili wa Mashahidi wa Yehova walinipa kitabu hiki.’ Kisha akaanza kulia, akilia kwikwi asijidhibiti. Katikati ya kwikwi, akasema: ‘Nimesoma kitabu hiki safari nyingi, na sura niliyorudia kusoma tena na tena ni “Unaweza Kukabilianaje na Msongo wa Marika?”’ Akaongeza hivi: ‘Laiti ningalikuwa na habari hii miaka mitatu au minne iliyopita, singalikuwa hapa leo.’

“Mfungwa huyo alipelekwa zake, nami nikasoma ripoti ya polisi na ungamo alilotoa kwa polisi. Katika hilo alisema: ‘Kiongozi wa genge langu aliniambia nishuke barabarani nikapige risasi mshiriki wa genge la wakinzani aliyekuwa akiuza bangi katika eneo letu. Mimi nilifanya nilivyoambiwa. Nilihofu washiriki wale wengine wangefikiri mimi si shujaa. Nilitaka kukubaliwa.’”

Labda wewe pia umejiuliza maswali kama: Naweza kukabilianaje na msongo wa marika? Je! niache shule? Naweza kukataaje ngono kabla ya ndoa? Kwa nini nikatae dawa za kulevya? Hizo ni baadhi tu ya habari zinazozungumzwa katika Questions Young People Ask—Answers That Work. ikiwa wapendezwa kupokea nakala ya kitabu hiki cha kurasa 320 chenye vielezi vya kuvutia, tafadhali jaza na kupeleka kuponi hii.

Ningependa kupokea kitabu chenye jalada gumu Questions Young People Ask—Answers That Work.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki