Kilitumiwa Katika Darasa la Mafunzo
Kitabu Life—How Did It Get Here? By Evolution or by Creation? kilitumiwa katika shule moja ya Kalifornia. Msichana wa miaka 11 aeleza kilivyotumiwa. “Mimi nilikuwa nikikitazama-tazama kitabu Creation kwa kukipitia,” yeye aandika, “nami nikaona kwamba zilikuwamo sura kadhaa kuhusu ulimwengu wote mzima na nyota. Wakati huo mwalimu wangu alikuwa amekuwa akitufundisha somo la nyota.
“Kwa hiyo nikaandika katika kipande cha karatasi sura ambazo yeye angeweza kuona shangwe kuzisoma, nikampa karatasi hiyo pamoja na kitabu hicho. Hakusema lolote kwa miezi kadhaa. Halafu akaanza kutufundisha juu ya ile nadharia ya kwamba vitu vilitokea ghafula kwa mshindo mkuu. Alisema kwamba alikuwa amekuwa akijifunza kitabu fulani. Alienda kwenye dawati lake akachomoa Life—How Did It Get Here? By Evolution or by Creation? Nilishangaa sana!
“Alisema kwamba kilikuwa ndicho kitabu bora kabisa alichopata kusoma. Halafu akafungua kitabu hicho na kuonyesha darasa picha zilizomo. Niliona kwamba alifanya ki-i-la swali lililo katika kitabu hicho lijibiwe na kukaziwa. Alipokuwa akitufundisha, alikuwa akifungua kitabu hicho, kusoma fungu, halafu kulieleza. Ulipokuja wakati wa mtihani, maswali yalitoka mle mle ndani ya kitabu hicho. Hivyo basi ilikuwa rahisi kwangu kujifunza nijitayarishe kwa mtihani huo. . . . Nilipata A.”
Sisi twahisi kwamba wewe pia waweza kunufaika na kitabu hiki. Ikiwa ungependa kupokea nakala, tafadhali jaza na upeleke hati ya anwani iliyoambatanishwa.
Mimi ningependa kukipokea kitabu chenye jalada gumu cha kurasa 256, Life—How Did It Get Here? By Evolution or by Creation?
Foto ya NASA