Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w90 12/15 uku. 25
  • “Pango la Wanyang’anyi” la Ki-Siku-Hizi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Pango la Wanyang’anyi” la Ki-Siku-Hizi
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
w90 12/15 uku. 25

“Pango la Wanyang’anyi” la Ki-Siku-Hizi

KATIKA gazeti Natural History, profesa wa asili za kibinadamu Colin Turnbull alisimulia maono yake akiwa mtalii katika Yerusalemu. Alisema kwamba “roho ya Krismasi” aliyokuwa ameanza kusitawisha “ilipoa upesi” alipoona maduka ya jiji “yakiwa yamejaa makorokoro yenye kuuzwa kwa bei za juu sana kwa wanunuzi (watalii) wa wakati wa Krismasi walioonekana wakitaka sana kununua.”

Turnbull alisema hivi juu ya “roho [yake] ya Krismasi”: “[Iliondolewa mbali] zaidi katika mahali pamoja ambapo nilifikiri ndipo ningeweza ku[i]fanya upya—kaburi la yale Mazikio Matakatifu.” (Sehemu ya ndani inaonekana pale juu.) Huko, mwenendo wa watalii wenzake “walioonekana wakionyesha wazi ukosefu mbaya sana wa heshima kwa vitu vitakatifu” ulimvunja moyo ‘walipokuwa wakisukumana na kujongezana kwa njia ya kukosa sana Ukristo, wakitumia mabega na viko vya mikono kujisukumiza wapite katika ule mwingilio mwembamba wa kwenda kwenye mazikio yenyewe. Pindi kwa pindi pigano dogo lilitokea, likiandamana na kuapa na vitendo ambavyo havikuwa kamwe vitakatifu.’

Badala ya “kurudisha hali ya utakato,” Turnbull akasema, makasisi wasimamizi “waliondolea mbali wazio lolote la utakatifu wao wenyewe walipoweka kielelezo cha kuwa na mwenendo wa matata.” Alisimulia juu ya “jamaa mmoja mwenye joho la kahawia, lenye kumfunika sana mpaka kichwani, akiwa kama Rasputin” ambaye “kwa ubeberu alikumba watalii wa kikawaida warudi nyuma kutoka mwingilio wa mazikio kila wakati ambapo kikundi cha watalii wenye kutoa malipo ya juu zaidi (wanaoitwa mapiligirimu), walipotokea wakiwa wameshika mishumaa inayowaka, bado wakiongozwa na Rasputin mwingine.” Tokeo, akasema mwelimishaji huyo, lilikuwa “uadui kati ya wasioshika mishumaa na wenye kushika mishumaa, na pia kati ya makasisi mbalimbali, kwa maana kulionekana kuwa na andamano lisilo na mwisho la madhehebu zenye kushindania wakati na nafasi.”

Mwandamani wa profesa Turnbull alikuwa “umbali wa yadi [meta] chache nyuma ya mahali hapo penye kuheshimiwa, akiwa amesujudu, akiwa amefichika nusu katika shimo ukutani.” Turnbull alisimulia hivi: “Nilipokuwa nikitazama, mkono wake ulitokeza nje ukapapasa kiupofu kutafuta pesa katika mfuko wake, lakini mkono wake ule mwingine ukabaki ndani, ukiwa umenyooshwa kana kwamba umeshikwa. Hata hivyo, alipokwisha kuhamisha pesa zile kuzirudisha ndani ya shimo, mkono wake wa kushoto uliachiliwa, na rafiki yangu akasimama . . . Katika mkono wake wa kushoto alishika msalaba mdogo sana wa mbao, ukiwa na unyevu mahali ulipokuwa umenyunyiziwa eti maji matakatifu na mtawa-mume mwenye haki ya kufanya hivyo ambaye alijikunja ndani ya lile pango dogo, akingojea windo lake.”

Yesu Kristo aliona mwenendo wa jinsi hiyo ukifanywa na watu mashuhuri hekaluni, naye akawaambia kwamba walikuwa wakiligeuza kuwa “pango la wanyang’anyi.” (Luka 19:45, 46) Bila shaka, katika siku yetu hayo ‘mapango ya wanyang’anyi’ hayako Yerusalemu tu.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 25]

Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki