Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w91 4/1 uku. 30
  • Siasa—Je! Ni Sehemu Ya Utume Wa Kueneza Gospeli?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Siasa—Je! Ni Sehemu Ya Utume Wa Kueneza Gospeli?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
w91 4/1 uku. 30

Siasa—Je! Ni Sehemu Ya Utume Wa Kueneza Gospeli?

KULINGANA na Joachim Meisner, askofu mkuu wa Cologne ambaye hapo kwanza alikuwa kasisi mashuhuri wa Ujeremani Mashariki, “ni uzushi kuziita siasa kuwa ni chafu, shughuli ambayo kwayo mtu huchafua mikono yake.” Katika mahoji mamoja ya 1989, alisema hivi: “Siasa ni uhalisi wa maisha na kwa hiyo ni sehemu ya utume wetu wa gospeli (habari njema). Ni lazima tukubali kukabiliana na dai hilo. Kwa njia chanya, ni lazima tupenye ndani ya kila shirika la kisiasa, kuanzia vyama vya wafanya kazi na mashirika hadi kwenye vyama vya kisiasa, kufanyiza katika harakati na vyama hivyo msingi wa uhalisi wa Ukristo ambao kutokana nao watu mmoja mmoja waweza kutokea ili wachukue uongozi katika kuendeleza siasa za Ujeremani na Ulaya.”

Manukuu yanayofuata kutokana na Frankfurter Allgemeine Zeitung, gazeti maarufu moja la Ujeremani, yaonyesha kwamba makasisi wengi wa Ulaya—Wakatoliki na Waprotestanti pia—hushiriki maoni ya Meisner.

“Siku sita tu baada ya kuchaguliwa kwake [Oktoba 1978], yeye [papa] alitangaza kwamba kwa kuwa yeye ni wa Ulaya ya Mashariki hakukusudia kukubali hali ya sasa ya kijamii katika Ulaya. . . . Watu fulani walichukua hayo kuwa mahubiri, lakini ilikuwa programu ya kisiasa.”—Novemba 1989.

“Katika mahali fulani [katika Chekoslovakia] kanisa lilipata heshima kubwa ya kuwa mtangulizi katika ule msukosuko. Wanafunzi kwenye seminari ya mapadri katika Litomerice, mji wa kaskazini wa Kibohemia wenye kathedro, . . . waliongoza mapinduzi yasiyo na jeuri ya Novemba uliopita.”—Machi 1990.

“Ile sala ya kila juma ya amani katika Kanisa la Nikolai [la Kiprotestanti], ambayo kwa miaka kumi haikuvuta fikira sana, kwa ghafula ikawa kifananisho cha mwaka huu cha msukosuko, cha mapinduzi yenye amani katika ile Jamhuri ya Ujeremani ya Kidemokrasi. . . . Makasisi wasiohesabika na waenda-kanisani hushiriki kwa ukawaida katika maandamano yenye kufanywa baadaye.”—Desemba 1989.

Katika mahoji yake Askofu Mkuu Meisner alisema hivi pia: “Hatuwezi kungojea wanasiasa Wakristo waanguke kutoka mbinguni. Mimi sichoki kamwe kuwatia moyo Wakristo wachanga . . . kuhusika katika maisha ya kisiasa [au ya] . . . kuambia raia wenye umri mkubwa hivi: Ni lazima msiruhusu uchaguzi wowote upite bila nyinyi kuhusika.”

Kwa hiyo, washiriki 19 wa Volkskammer (bunge) la Ujeremani ya Mashariki ambao walipigiwa kura kuingia cheoni katika Machi 1990 walikuwa makasisi. Dini pia iliwakilishwa katika baraza la mawaziri. Kuhusu mmoja wa makasisi wayo watatu, Waziri wa Ulinzi Rainer Eppelmann, mwenye kushikilia sana amani, gazeti Nassauer Tageblatt liliandika hivi: “Wengi humwona kuwa mmoja wa mababa wa mapinduzi yenye amani.”

Mashahidi wa Yehova katika Ulaya ya Mashariki, ambao hesabu yao inaingia mamia ya maelfu, waushangilia uhuru wa kidini walio nao sasa. Lakini hawautumii kuhusika katika mabishano ya kisiasa au ya kijamii. Kupatana na utume wa kueneza gospeli ambao wasemwa kwenye Mathayo 24:14, wao wanafuata kielelezo cha Yesu cha kuepuka kabisa siasa za kibinadamu, muda wote huo wakihubiri kwa bidii habari njema za Ufalme wa Mungu kuwa ndio tumaini pekee la ainabinadamu. Makasisi wa Jumuiya ya Wakristo—iwe ni katika Ulaya ya Mashariki au kwingineko—wangekuwa wenye hekima kutenda hivyo hivyo.—Yohana 6:15; 17:16; 18:36; Yakobo 4:4.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki